• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na rais Putin wa Russia

    (GMT+08:00) 2014-02-07 09:32:56
    Rais Xi Jinping wa China jana alikutana na rais Vladimir Putin wa Russia huko Sochi, Russia. Rais Xi alisema anafurahi kuhudhuria ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya Sochi kutokana na mwaliko wa rais Putin. Rais Xi alisema ni furaha kubwa kwa Russia kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Sochi, wakati Wachina wanasherehekea Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi. Amesema michezo ya Olimpiki ya Sochi ni ishara kuwa rais Putin anawaongoza Warussia kwa ajili ya ustawi zaidi. Rais Xi Jinping alisema, China na Russia ni majirani wema na marafiki wakubwa. Kwa mujibu wa mila na desturi za China, jirani akiandaa sherehe, bila shaka atapongezwa ana kwa ana. Ameitakia michezo hiyo mafanikio, na kuwatakia wachezaji wa China na Russia wapate ushindi.

    Rais Putin amemkaribisha na kumshukuru sana rais Xi Jinping kuhudhuria ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Sochi. Amesema sikukuu ya mwaka mpya ya jadi ya China ni siku ya kuwatembelea jamaa na marafiki, kwa hiyo rais Xi Jinping amekwenda Russia kumtembelea rafiki mkubwa. Amemtakia rais Xi na Wachina heri ya mwaka mpya wa jadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako