• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na mwenyekiti wa kamati ya kimataifa ya Michezo ya Olimpiki

    (GMT+08:00) 2014-02-07 15:59:12
    Rais Xi Jinping wa China jana usiku alikutana na mwenyekiti wa kamati ya kimataifa ya Michezo ya Olimpiki Bw. Thomas Bach huko Sochi, Russia.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, serikali ya China inatilia maanani na kuunga mkono Michezo ya Olimpiki ya kimataifa. Baada ya michezo ya Olimpiki ya Beijing kufanyika kwa mafanikio, China inagombea kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi ya mwaka 2020, hii itahimiza kuenea na kukuza michezo ya majira ya baridi nchini China. Rais Xi ameongeza kuwa, sekta ya michezo imepata maendeleo makubwa nchini China, na China itaimarisha kiwango chake cha michezo na kuendelea kuwahimiza watu wake kufanya mazoezi zaidi.

    Naye Bw. Bach ameeleza imani yake kuwa, kwa kugombea kuwa mwenyeji wa michezo ya olimpiki ya majira ya baridi ya mwaka 2020, China itaimarisha uwezo wake wa michezo ya barafu. Amesema kamati ya kimataifa ya Michezo ya Olimpiki inafurahia maandalizi ya Michezo ya Olimpiki ya vijana ya awamu ya pili itakayofanyika mjini Nanjing, China mwezi Agosti mwaka huu.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako