• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Awamu ya 22 ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya mwaka 2014 yafunguliwa rasmi mjini Sochi

    (GMT+08:00) 2014-02-08 10:45:00

    Tarehe 7 Februari kwa saa za huko, awamu ya 22 ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya mwaka 2014 ilifunguliwa rasmi kwenye Uwanja wa Michezo wa Olimpiki wa Fisht mjini Sochi, Urusi.

    Rais wa Urusi Vladimir Putin alitangaza kufunguliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi. Viongozi wa nchi na sehemu zaidi ya 40 akiwemo Rais Xi Jinping wa China na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon walihudhuria sherehe hiyo ya ufunguzi.

    Awamu hiyo ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ilianzisha michezo ya aina kubwa 15 na aina ndogo 98. Kwa jumla wanamichezo zaidi ya elfu 3 wanaotoka nchi na sehemu 87 watahudhuria michezo hiyo. China imetuma ujumbe wenye watu 139 kushiriki michezo hiyo, wakiwemo wanamichezo 66. Mwanamchezo maarufu wa kuteleza barafu wa China Tong Jian ambaye aliwahi kupata medali ya fedha kwenye awamu iliyopita ya Michezo ya Olimpiki atashika bendera ya kitaifa ya China kwenye sherehe hiyo ya ufunguzi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako