• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya rais Xi Jinping wa China mjini Sochi, Russia yafungua ukurasa mpya wa kidiplomasia nje ya China

    (GMT+08:00) 2014-02-09 19:35:57

    Kwa kufuatia mwaliko wa rais Vladimir Putin wa Russia, rais Xi Jinping wa China amefanya ziara ya siku 3 na kuhudhuria ufunguzi wa Michezo ya 22 ya Olimpiki ya Majira ya Baridi mjini Sochi, Russia.

    Akizungumzia ziara hiyo mjini Sochi, waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi amesema ziara hiyo imeonesha uungaji mkono mkubwa wa China kwa Russia katika kuandaa michezo ya Olimpiki ya majira ya baridi, na pia imepanga mpango wa kimkakati kwa ajili ya China na Russia kuendeleza uhusiano wao katika mwaka mpya.

    Wakati wa ziara hiyo, rais Xi Jinping alifanyiwa mahojiano maalumu na televisheni ya taifa ya Russia, ambapo ameeleza matumani ya kuimarisha ushirikiano wa kirafiki na Russia, na pia kufafanua mustakabali mzuri wa China baada ya kutekelezwa kwa sera ya mageuzi na ufunguaji mlango.

    Bw. Wang Yi amesisitiza kuwa ziara hiyo imeonesha kuwa China inatilia maanani na kuunga mkono michezo ya Olimpiki ya kimataifa. Rais Xi pia ametoa salamu kwa wanamichezo wa Kichina kwa niaba ya watu wa China.

    Katika ziara hiyo, rais Xi pia amefanya mazungumzo na marais wa Czech, Ugiriki na Afghanistan pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon, na pia ameongea na wakuu wa nchi 40 na mashirika mbalimbali ya kimataifa ya michezo. Hatua hiyo imesaidia kuhimiza maelewano na ushirikiano wa kirafiki kati ya China na pande mbali mbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako