• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatangaza sekta 9 muhimu za uendelezaji wa sehemu ya magharibi mwa China katika mwaka huu

    (GMT+08:00) 2014-02-10 16:54:19

    Kamati ya maendeleo na mageuzi ya China leo imetangaza sekta 9 muhimu za uendelezaji wa mikoa 12 ya magharibi mwa China. Sekta hizo ni pamoja na kuharakisha ujenzi wa miundo mbinu zikiwemo mawasiliano ya barabarani na maji, kuanzisha duru mpya ya mradi wa kubadili mashamba kuwa misitu; kuhimiza maendeleo ya shughuli maalum; na kuendeleza shughuli za sayansi, teknolojia, utamaduni, na maisha ya watu, ili kuboresha mazingira ya uzalishaji na maisha ya watu.

    Sehemu ya magharibi mwa China inachukua asilimia 71 ya eneo la China, na idadi ya watu imezidi milioni 360, lakini uchumi na jamii ya sehemu hiyo havijaendelezwa kama ilivyo sehemu ya mashariki. Ili kupunguza tofauti hiyo, mwaka 1999 China ilitangaza mkakati wa uendelezaji wa sehemu ya magharibi. Katika miaka 10 iliyopita, uchumi na jamii ya sehemu hiyo zikiwemo mikoa ya Ningxia na Tibet zimepata maendeleo ya kasi, mazingira ya viumbe yameboreshwa, na kiwango cha maisha ya watu wa huko kimeinuliwa kwa kasi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako