• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FAO Huenda kenya ikakumbwa na uhaba wa nafaka

    (GMT+08:00) 2014-02-12 09:43:03
    Ripoti ya shirika la umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO inasema kwamba kupungua kwa mvua huenda kusababisha uhaba wa nafaka nchini Kenya.

    Ripoti hiyo inatolewa wakati tayari zaidi ya watu milioni mbili nchini humo wakikabiliwa na njaa na mifugo ikikosa lishe.

    Ronald Mutie anaripoti.

    Hapa ni katika eneo la Kitui mashariki mwa kenya.

    Hili ni mojawepo wa maeneo ambayo yamekosa mvua na mimea yote imekauka shambani.

    Shule za karibu zimelazimika kufungwa kutokana na ukosefu wa chakula.

    Wakaaazi wanasema kwa muda sasa hawajapokea chakula cha msaada kutoka kwa serikali ama kwa mashirika.

    Maji pia yameadimika na machache yaliomo yanauzwa kwa bei ghali.

    Lakini sio ukosefu wa mvua tu unaosababisha ukosefu wa chakula.

    Katika eneo la bonde la ufa ambako kuna mvua ya kutosha mahindi yameathiriwa na ugonjwa wa Necrosis na mavuno ni haba.

    Na huku hali hi ikizidi kukithiri shirika la chakula na kilimo FAO linaonya kwamba maeneo yanayozalisha nafaka yatakuwa na upungufu wa hadi asilimia 11 ikilinganishwa na mwaka jana.

    Kulingana na FAO baadhi ya maeneo yaliyoathirika ni pamoja na kusini mashariki na pwani ambako kuchelewa kwa msimu wa mvua mwaka jana kulichelewesha shughuli za upanzi huku nacho kiangazi kilichofuatia kikiathiri mavuno.

    Katika maeneo hayo asilimi 65 ya mimea hutegemea sana mvua na sasa nafaka kama vile mahindi huenda ikapungua.

    Kulingana na afisa wa Chakula kutoka shirika hilo la FAO nchini kenya Bwana Simon muhindi uzalishaji wa mahindi unatarajiwa kuwa kati ya asilimia 30 na 40 chini ya wastani.

    "Katika maeneo muhimu ya uzalishaji wa chakula tutakuwa na upungufu wa nafaka wa kati ya asilimia 30 na 40 kutokana na kiangazi. Pia mahindi ambayo ni lishe kuu la wakenya yameathirika na maradhi na hilo pia ni jambo lilaloleta wasiwasi kwetu"

    Muhindi anasema pia shirika hilo limetoa dola 280, 000 kusaidia kufanya utafiti wa kiwango cha chakula nchini.

    Utafiti huo utafanywa katika kaunti 24 zinazozalisha chakula kwa wingi kote nchini.

    Bwana Joseph matere ni afisa wa mawasiliano wa maswala ya kijiografia kutoka FAO.

    "Hii itatusaidia kupata taakwimu kuhusu kiwango cha chakula tulichonacho hivi sasa na pia kukadiria tutakuwa na kiasi gani ndani ya miezi sita ijayo. Kutokana na utafiti huo pia serikali itaweza kujua iwapo itaagizia nafaka ama tuna chakula cha kutosha"

    Idadi ya zaidi ya watu milioni 40 nchini kenya hutumia magunia milioni nne ya mahindi kila mwezi huku mahitaji ya kila mwaka ya nafaka yakiwa ni magunia milioni 48.

    Serikali tayati imetoa tahadhari ya kiangazi na inatoa wito kwa wakulima wa mifugo kupunguza mifugo yao ili kuepuka hasara kutokana na ukosefu wa lishe.

    Bi. Kadijah Kassachoon ni katibu wa kudumu katika wizara ya mifugo.

    "Tumetoa tahadhari kwa magavana wote kwamba wafugaji wanafaa kupunguza mifugo walio nayo.Pia tumehakikisha kwamba tume ya nyama nchini yaani KMC inanunua baadhi ya mifugo hiyo ili kupunguza shinikizo kwenye malisho"

    Tayari serikali ya kenya imetumia shilingi milioni mia sita katika mipango ya kutoa chakula cha misaada ya chakula kwa waanga wa njaa.

    Rais uhuru Kenyatta anasema kwa jumla serikali imetenga shilingi bilioni 4.3 za kukabiliana na kiangazi mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako