Baraza la Nafaka Afrika Mashariki (EAGC) limetoa wito wa kuwekwa utaratibu utakaowezesha ukuaji wa nafaka wa kikanda unaoendelea ili kukuza uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katika mkutano jijini Nairobi ulioandaliwa na shirika la East Africa Commodity Exchange Mwenyekiti wa EAGC Judah arap Bett ametoa wito kwa serikali za Afrika Mashariki kuendelea kushirikiana na sekta binafsi katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto walizo nazo,na kutunga sera zitakazojenga mazingira mazuri kwa sekta binafsi kustawi.
Mkutano huo ulinuiwa kuitambulisha East Africa Commodity Exchange kwa wafanyabiashara wa nafaka wa Kenya na wadau wengine katika sekta ya kilimo na fedha katika soko la Kenya .
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |