Rais Barack Obama wa Marekani amesisitiza umuhimu wa maendeleo ya kiuchumi na ushirikiano kwa Amerika ya Kaskazini.
Hayo ameyasema wakati alipohudhuria mkutano wa viongozi wa Amerika ya Kaskazini huko Mexico. Rais Obama amesema, mkutano huo uliowashirikisha rais Enrique Pena Nieto wa Mexico na waziri mkuu wa Canada Stephen Harper unalenga kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizi tatu, na kuongeza kuwa nchi hizo zina kanuni za pamoja ikiwemo demokrasia na biashara huria.
Pia amesema, biashara huria kati ya nchi hizi tatu itaruhusu nchi hizo kuuza bidhaa zao na kutoa huduma zao duniani kote.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |