• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Ukraine lamuondoa madarakani rais Victor Yanukovich wa Ukraine

    (GMT+08:00) 2014-02-23 19:17:24

    Bunge la Ukraine leo limepiga kura ya kumuondoa madarakani rais Victor Yanukocich na kumuachia huru aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Yulia Tymoshenko baada ya miezi mitatu ya vurugu na maandamano nchini humo. Yanukovich ambaye alisisitiza kuwa hataondoka madarakani anadaiwa kuuhama mji mkuu wa Kiev na kukimbilia sehemu ya kusini yenye watu wengi wanaomuunga mkono. Muda mfupi baada ya kutoka gerezani, Tymoshenko alifika kwenye uwanja wa Uhuru na kuwahutubia waandamanaji. Yanukovich ameonya kuwa hatakubali uamuzi wowote wa bunge na amewataja viongozi wa upinzani kuwa genge la wahuni ambalo limekuwa likiwaangaisha watu wa Ukraine. Wakati huohuo, bunge la nchi hiyo limemteua Bw Alexandr Turchonov kuwa spika mpya wa bunge la Ukraine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako