• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaeleza hali ya utungaji wa sheria kwa mwaka jana

    (GMT+08:00) 2014-02-25 17:06:14

    Bunge la Umma la China litaitisha mkutano wa mwaka hivi karibuni, na kabla ya kufanyika kwa mkutano huo, maofisa wa idara inayoshughulikia mambo ya sheria katika Kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China wamefafanua kazi walizofanya katika mwaka jana.

    Kutunga sheria ya utalii ni moja ya kazi muhimu zilizofanywa na Kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China la awamu mpya katika mwaka 2013. Hii ni sheria ya kwanza ya utalii ya China, na pia ni sheria ya kwanza iliyopitishwa na kamati hiyo. Kabla ya kutolewa kwa sheria hiyo, masuala mbalimbali katika soko la utalii la China ikiwemo kulazimisha watu kulipia ada kubwa ya vingilio yanalalamaikiwa sana. Msafiri mmoja anasema, "shirika la utalii linatulazimisha tununue vitu wakati tunasafiri, lakini sisi tunataka kutumia pesa tunavyopenda. Ni lazima ukaguzi mkali ufanyike dhidi ya sekta ya utalii, ili sekta hii iweze kustawi baada ya kurekebishwa."

    Baada ya kusikia wito wa watu, watunga sheria walifanya sensa na kusikiliza maoni ya pande mbalimbali ili kujua hali ilivyo katika jamii ya China. Akizungumzia uchunguzi wa kisiri waliofanya, naibu mkurugenzi wa ofisi ya sheria ya uchumi katika Kamati ya kudumu ya Bunge la Umma la China ambaye alishiriki kwenye utungaji wa sheria ya utalii Bw. Yang Heqing anasema, "Tulifanya uchunguzi na kuwasiliana na wafanyakazi wa shirika la utalii kama watalii wa kawaida, tulipotembelea sehemu mbalimbali tuliongea na wafanyakazi wa vivutio vya utalii na wakazi, tukijadiliana nao kuhusu hali ya soko la utalii. Tulijionea hali nyingi halisi na kusikia maoni mengi halisi, hii ilitusaidia sana."

    Ikiwa ni sehemu isiyoweza kuachwa katika kutunga sheria, sensa inalenga kupunguza udhaifu na upofu. Mbali na sensa na mazungumzo, kamati ya kudumu ya Bunge la umma la China ilisikiliza maoni kuhusu mswada wa sheria kupitia mtandao wa internet. Mwaka jana walipojadili kurekebisha sheria ya uhifadhi wa mazingira, waliomba maoni mara 2 kwa jamii, hatua ambayo ni nadra kutokea katika siku zilizopita. Naibu mkuu wa ofisi ya utafiti ya kazi ya mambo ya sheria katika kamati ya kudumu ya bunge la umma la China Liang Ying anasema, "Tutafanya kuomba maoni mara mbili kuwa utaratibu, na kama sheria ni muhimu, na inahusiana na maisha ya watu na kufuatiliwa na watu wa kawaida, labda tutaomba maoni mara tatu katika siku za baadaye."

    Baada ya kupitia sheria zilizotungwa na zile zilizorekebishwa na kamati ya kudumu ya bunge la umma la China mwaka jana, ni wazi kuwa kazi ya utungaji sheria imezingatia zaidi ufanisi, na vipengele vya sheria vimekuwa wazi zaidi. Kwa mfano, katika kusikiliza marekebisho ya sheria ya uhifadhi wa mazingira, walisisitiza haki ya watu kujua, kushiriki na kusimamia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako