• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kazi ya usimamizi ya Bunge la 12 la Umma la China yatoa ufanisi

    (GMT+08:00) 2014-02-26 17:47:06

    Usimamizi ni kazi muhimu ya Bunge la Umma la China kwa mujibu wa katiba. Mwaka jana Bunge la Umma la China na kamati yake ya kudumu ziliimarisha usimamizi wa kazi na hali ya utekelezaji wa sheria katika serikali, mahakama na idara ya uendeshaji mashtaka, wakizungumza na wakazi, kutuma fomu za sensa na kuomba maoni ili kufanya uvumbuzi kuhusu njia za usimamizi, na kazi za usimamizi za Bunge la Umma la China la awamu mpya zimekuwa na ufanisi zaidi. Fadhili Mpunji ana maelezo zaidi.

    Kwa mujibu wa mwaliko wa Kamati ya kazi ya bajeti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la umma la China, mwanzoni mwa mwaka huu mkulima wa wilaya ya Qianguo mkoani Jilin Tan Yejun alifika Beijing kwa mara ya kwanza baada ya kuishi nusu ya maisha yake na kushiriki katika majadiliano kuhusu usimamizi wa bajeti yaliyoandaliwa na Wizara ya Kilimo.

    Kabla ya kufanyika kwa mikutano miwili ya Bunge la Umma la China na Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China kila mwaka, Kamati ya kazi ya bajeti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la umma la China ilishirikisha Wizara ya Fedha na wizara nyingine kufanya mazungumzo kuhusu kazi ya usimamizi wa bajeti, na kutoa mapendekezo na maoni kuhusu bajeti yaliowasilishwa kwa bunge la umma la China wakati wa mikutano hiyo miwili, ili kufanya bajeti ya taifa kuitikia maoni na kujibu matarajio ya wakazi wa kawaida, kabla ya kufanyika kwa mikutano miwili ya mwaka huu, Kamati ya kazi ya bajeti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la umma la China iliwawaalika wajumbe wa wakazi akiwemo Bw. Tan Yejun kwenye majadiliano hayo.

    Kwenye mkutano huo, Bw. Tan alitaja masuala yanayokwamisha ukuaji wa mapato ya wakulima wa nafaka ikiwemo kupanda polepole kwa ruzuku na ruzuku ndogo katika kununua mashine. Mkurugenzi wa ofisi ya usimamizi ya bajeti ya kamati ya kazi ya bajeti ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la umma la China aliyeendesha majadiliano hayo alisema, maoni ya Bw. Tan yanatia moyo. Njia hiyo ya kuwashirikisha watu wa kawaida kwenye kazi ya usimamizi wa bajeti itaisaidia kazi ya usimamizi wa bajeti ya Bunge la Umma la China kuonesha busara ya watu na maoni ya watu.

    Usimamizi wa hali ya utekelezaji wa sheria na utaratibu na kazi nyingine muhimu ya mamlaka ya usimamizi wa Bunge la Umma la China. Ikiwa ni njia moja ya kisheria ya watu kumshitaki ofisa wa serikali, sheria ya uangalizi mpya wa kiutawala imefanya kazi kubwa tangu itolewe mwaka 1999, lakini pia kuna masuala mengi zikiwemo kutopitika kwa njia za uangalizi mpya, au hali ya watu kutokuwa waaminifu. Ili kufahamu hali ya utekelezaji wa sheria hiyo na matatizo yaliyopo, Bunge la Umma la China lilitoa fomu 5,000 za sensa kwa watu wanaoishi katika wilaya 1400 za mikoa 15, nchini kote, na kuomba maoni yao kupitia tovuti ya Bunge la umma la China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako