• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaamua Siku ya kuadhimisha ushindi katika Vita dhidi ya Wajapani na Siku ya Kuwakumbuka waliouawa katika Mauaji ya Nanjing

    (GMT+08:00) 2014-02-27 17:05:07

    Bunge la Umma la China ambalo ni chombo cha kutunga sheria nchini China leo limepitisha azimio la kufanya tarehe 9 Septemba kuwa Siku ya Kuadhimisha Ushindi wa Wananchi wa China katika Vita dhidi ya Wajapani na tarehe 13, Desemba kuwa Siku ya Kuwakumbuka watu waliouawa katika Mauaji ya Halaiki ya Nanjing. Azimio hilo linatokana na hoja zilizotolewa na wajumbe wa bunge kwa miaka mingi. Wakizungumza na waandishi wa habari, wajumbe hao waliowahi kutoa hoja hizo walisema azimio hilo limeitikia matakwa ya wananchi, kuonesha nia ya China ya kupata amani na pia linalingana na utaratibu wa kimataifa.

    Katika mkutano wa Bunge la Umma la China uliofanyika mwaka 2012, mjumbe wa bunge Bw. Zou Jianping alitoa hoja ya kuwepo kwa Siku ya kitaifa ya Kuwakumbuka watu waliouawa katika Mauaji ya Halaiki ya Nanjing. Akizungumzia sababu ya kutoa hoja hiyo, Bw. Zou alisema ametafakari jambo hilo kwa miaka mingi, lakini tukio moja lililotokea mwaka 2012 lilimhimiza atoe hoja hiyo.

    "Mji wa Nagoya na mji wa Nanjing ni miji "ndugu", lakini mwaka 2012, meya wa mji wa Nagoya alikana hadharani kutokea mauaji ya halaiki ya Nanjing, hii haiwezi kukubaliwa na watu wa Nanjing na hata watu wa China. Hii ndio sababu iliyonifanya nitoe hoja hiyo."

    Kuweka siku ya taifa ya maadhimisho kwa kupitia sheria ni hatua inayokubalika duniani. Russia na Ukraine zote zimeweka siku ya kuadhimisha ushindi wa vita kwenye sheria, na siku ya kuadhimisha mauaji ya halaiki ya Israel pia imewekwa kwenye sheria. Naibu mkuu wa jumba la makumbusho ya vita ya Wachina dhidi ya uvamizi wa Wajapani Bw. Li Zongyuan amesema, kuamua Siku ya Kuadhimisha Ushindi wa Wananchi wa China katika Vita dhidi ya Wajapani na Siku ya Kuwakumbuka Watu Waliouawa katika Mauaji ya Halaiki ya Nanjing kwenye sheria, si kama tu imeonesha ufuatiliaji mkubwa wa serikali ya China, bali pia ni pigo kubwa dhidi ya watu wenye siasa kali ya mrengo wa kulia nchini Japan wanaokataa na kupotosha historia.

    Wakati hali ya uhusiano kati ya China na Japan ikizidi kuwa mbaya, kuna watu wanaodai kuwa serikali ya China kutunga sheria kuweka Siku ya Kuadhimisha Ushindi wa Wananchi wa China katika Vita dhidi ya Wajapani na Siku ya Kuwakumbuka Watu Waliouawa katika Mauaji ya Halaiki ya Nanjing ni hatua ya kidiplomasia dhidi ya Japan. Akizungumzia kauli hiyo, mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa historia ya zama za hivi karibuni katika Taasisi ya Jamii na Sayansi ya China Bw. Wang Jianlang anasema hatua hiyo haiilengi tu Japan, hii inatokana na historia na nia ya kutafuta amani ya China.

    (sauti 5) "China imetoa mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya ufashisti, kuweka siku ya kuadhimisha ushindi wa vita kuna sababu za kihistoria. Hatua hiyo inaonesha kuwa serikali ya China inapenda amani badala ya vita, na inakumbuka madhara ya vita na kujitahidi kuzuia vita isitokee."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako