• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa pili wa baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China kufunguliwa kesho mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2014-03-02 19:10:02

    Mkutano wa pili wa baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China unatarajiwa kufunguliwa kesho alasiri katika Jumba la mikutano ya umma mjini Beijing.

    Zaidi ya wajumbe elfu 2 wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la China watasikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya baraza hilo, pamoja na ripoti ya baraza hilo kuhusu utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano wa kwanza wa baraza hilo.

    Habari zinasema , Radio ya taifa ya China CNR, Televisheni ya taifa ya China CCTV, na Radio China Kimataifa CRI zitatangaza moja kwa moja ufunguzi wa mkutano huo, pamoja na ripoti ya kazi ya kamati ya kudumu ya baraza la mashauriano ya kisiasa la China itakayotolewa na mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Yu Zhengsheng. Aidha tovuti muhimu za habari za taifa pia zitatoa ripoti kuhusu mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako