• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2014-03-03 15:47:18

    Mkutano wa mwaka wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China umefunguliwa katika Jumba la Mikutano ya Umma mjini Beijing, ambapo viongozi wa China akiwemo rais Xi Jinping na waziri mkuu Li Keqiang wameshiriki.

    Mkutano huo umeanza kwa wajumbe wanaohudhuria mkutano huo kuwakumbuka watu waliouawa katika tukio la kigaidi lililotokea tarehe 1 Machi kwenye kituo cha treni kilichoko Kunming, mkoani Yunnan. Mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Yu Zhengsheng ametoa ripoti ya kazi ya baraza hilo, na kueleza utekelezaji wa kazi katika mwaka uliopita, na kuweka mipango ya kazi kwa mwaka huu.

    Mkutano huo unatarajiwa kufungwa asubuhi ya tarehe 12. Wajumbe zaidi ya 2,100 wa baraza hilo watatoa mapendekezo kuhusu masuala muhimu ya sekta za siasa, uchumi, na maisha ya jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako