• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China imekuwa nchi kubwa zaidi ya kibiashara duniani

    (GMT+08:00) 2014-03-03 16:25:24
    Wizara ya biashara ya China, leo imetoa makala iliyoandikwa na waziri wake Bw. Gao Hucheng kwenye tovuti yake akisema, kwa mara ya kwanza China imekuwa nchi kubwa ya kwanza kibiashara duniani mwaka 2013.

    Takwimu kutoka shirika la biashara duniani WTO zinaonesha kuwa, mwaka jana, thamani ya jumla ya bidhaa zilizouzwa nje ya China na zilizoagizwa kutoka nchi za nje ilikuwa dola za kimarekani trilioni 4.16, ambayo imeizidi ile ya Marekani. Hii ni mara ya kwanza kwa nchi inayoendelea kuwa nchi kubwa zaidi ya kibiashara duniani.

    Bw. Gao ameongeza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, biashara na nchi za nje imechangia kiasi cha asilimia 18 kwa ongezeko la uchumi nchini China, na China imekuwa mwenzi mkubwa zaidi ya biashara wa nchi na sehemu zaidi ya 120.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako