• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2014-03-03 18:57:01

    Mkutano wa mwaka wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China umefunguliwa katika Jumba la mikutano ya umma mjini Beijing, ambapo viongozi wa China akiwemo rais Xi Jinping na waziri mkuu Li Keqiang wamehudhuria. Mkutano huo umeanza kwa wajumbe wanaohudhuria mkutano huo kuwakumbuka watu waliouawa katika tukio la kigaidi lililotokea tarehe 1 Machi kwenye kituo cha treni kilichoko Kunming, mkoani Yunnan. Mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Yu Zhengsheng ametoa ripoti ya kazi ya baraza hilo, na kueleza utekelezaji wa kazi katika mwaka uliopita, na kuweka mipango ya kazi kwa mwaka huu.

    Mkutano huo unatarajiwa kufungwa asubuhi ya tarehe 12. Wajumbe zaidi ya 2,100 wa baraza hilo watatoa mapendekezo kuhusu masuala muhimu ya sekta za siasa, uchumi, na maisha ya jamii. Mwenyekiti wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Yu Zhengshen, katika ripoti aliyotoa wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha mkutano wa 12 wa Baraza hilo amejumuisha baadhi ya mapendekezo muhimu yaliyotolewa na wajumbe wa mkutano huo katika mwaka uliopita, amesema

    "Wajumbe walitoa mapendekezo muhimu yakiwemo mchanganyiko wa ubunifu wa mfumo wa makampuni, ubunifu wa sayansi na teknolojia na ubunifu wa uendeshaji, kuendeleza uchumi wa aina mbalimbali, kuhimiza uwiano wa maendeleo ya makampuni ya kitaifa na binafsi, na kukamilisha utaratibu wa kujadili mishahara ya wafanyakazi kwa pamoja."

    Katika mwaka uliopita, wajumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa, washiriki wa baraza hilo na kamati mbalimbali zilitoa mapendekezo zaidi ya 5,000 kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo ya uchumi na jamii nchini China, na kutoa mchango muhimu kwa serikali. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya kazi ya wizara ya nguvukazi na huduma za jamii ya China Bw. Zheng Xuanbo amesema,

    "Wajumbe wanafuatilia sana huduma za jamii, hivyo tumejitahidi kubuni mpango wa bima ya uzeeni. Hivi sasa baraza la serikali la China limeamua kutekeleza mfumo wa bima ya uzeeni kwa ajili ya wakazi wa mijini na vijijini."

    Kuhusu kazi ya wajumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa la kwa mwaka huu, mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Yu Zhengsheng anasema:

    "Baraza hilo linatakiwa kutoa mapendekezo kwa kufuata hatua muhimu za mageuzi, kuhimiza uchumi kupata maendeleo, pamoja na masikilizano na utulivu wa jamii, kuonesha vya kutosha kazi ya baraza hilo ya kutoa njia muhimu ya kidemokrasia kwa wananchi kufanya majadiliano. Kufanya uchunguzi na utafiti kwa kina kuhusu kuendeleza uchumi wa umiliki wa pamoja, kukamilisha mfumo wa soko la fedha, kukamilisha utaratibu wa utandawazi wa miji, na mageuzi ya mfumo wa matibabu na afya, ili kusaidia serikali na chama kutoa sera zinazohusika."

    Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya Bw. Yu Zhengsheng, baraza la mashauriano ya kisiasa la China litatekeleza mpango wa kazi ya baraza hilo ya mwaka 2014. Ikilinganishwa na mwaka jana, ripoti hiyo pia imesisitiza kuongeza uwezo wa utekelezaji wa kazi ya baraza hilo. Bw. Yu Zhengsheng anasema:

    "Baraza la mashauriano ya kisiasa la China likiwa njia muhimu ya kidemokrasia kwa wananchi kufanya majadiliano, inatakiwa kutoa sehemu nyingi nzuri zaidi kufanya majadiliano. Kugundua matatizo kwa kufuata hali halisi, kufanya utafiti kuhusu matatizo hayo, kuheshimu tofauti na kutafuta makubaliano, kufanya majadiliano kwa njia ya kidemokrasia, na kutoa maoni na mapendekezo mwafaka. Pia inatakiwa kufanya juhudi za kuwawezesha wajumbe wote kuonesha kazi yao katika baraza hilo, na kujenga utaratibu wa kisayansi wa mfumo wa majadiliano ya kisiasa ya umma. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako