• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Thamani ya jumla ya bidhaa zilizouzwa nje ya China na kampuni binafsi yazidi dola za kimarekani bilioni 900 mwaka 2013

    (GMT+08:00) 2014-03-04 17:02:56
    Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na shirikisho la sekta za viwanda na biashara la China zinaonesha kuwa, thamani ya bidhaa zilizouzwa katika nchi za nje na kampuni binafsi za China ilifikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 910, ambayo imeongezeka kwa asilimia 19, huku thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nchi za nje na kampuni hizo ikifikia zaidi ya dola za kimarekani bilioni 5,700, ambayo imeongezeka kwa asilimia 28.

    Habari zinasema kuwa, mwaka jana China iliunga mkono kwa kiasi kikubwa zaidi maendeleo ya kampuni binafsi zinazofanya biashara na nchi za nje, na kuzisaidia kampuni hizo kupitisha bidhaa kwenye forodha, kukusanya mitaji, na kurudisha ushuru, pia kuzisaidia kupanua soko duniani. Takwimu hizo pia zinaonesha kuwa, mwaka 2013 thamani ya bidhaa zilizouzwa nje ya China na kampuni binafsi ilichukua zaidi ya asilimia 40 ya thamani ya bidhaa zilizouzwa katika nchi za nje na kampuni zote nchini China.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako