• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China kufunguliwa

    (GMT+08:00) 2014-03-04 18:09:13

    Mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China utafunguliwa tarehe 5 Machi, ambapo wajumbe zaidi ya elfu mbili wa bunge hilo kutoka sehemu mbalimbali za China watashiriki. Mkutano wa kwanza na waandishi wa habari wa mkutano huo umefanyika leo asubuhi ambapo msemaji wa mkutano huo Bibi Fu Ying amejibu maswali kuhusu masuala yanayofuatiliwa sana na watu.

    Katika Mkutano huo, Bibi Fu Ying amefahamisha kwanza kuwa mkutano wa bunge la umma la China utafunguliwa asubuhi ya tarehe 5 na kufungwa asubuhi ya tarehe 13. Mkutano huo utasikiliza na kujadili ripoti ya kazi ya serikali, kukagua na kupitisha ripoti kuhusu mipango, pamoja na ripoti ya bajeti. Kikiwa ni chombo cha juu cha utungaji wa sheria la China, bunge la umma la China linaonesha kazi muhimu katika mchakato wa kuendeleza mageuzi. Bibi Fu Ying amesema, bunge la umma la China litaongoza hatua za mageuzi kwa kufuata sheria. Anasema:

    "Maana ya kuongoza mageuzi kwa kufuata sheria ni kutunga, kurekebisha na kuondoa sheria zinazohusika kwa kufuata mambo muhimu ya mageuzi yanayofuatiliwa na wananchi, ili kuzifanya hatua zote za mageuzi kufanyika kwa kufuata sheria."

    Habari zinasema halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la China imeweka mipango mipya ya miaka mitano kuhusu utungaji wa sheria. Kati ya masuala mbalimbali, suala la uhifadhi wa mazingira linafuatiliwa zaidi.Mwanzoni mwa mwaka huu, baadhi ya miji mikubwa ya China imekumbwa tena uchafuzi mkubwa wa hewa. Akizungumzia suala hilo, Bibi Fu Ying ameeleza kuwa, hili ni tatizo kubwa linaloikabili baadhi ya miji nchini China. Bunge la umma la China litarekebisha sheria kuhusu uhifadhi wa mazingira, ili kutoa uhakikisho wa kisheria kwa kazi ya kushughulikia tatizo hilo. Bibi Fu anasema:

    "Katika mipango ya utungaji wa sheria katika halmashauri ya kudumu ya bunge la umma la China, utungaji wa sheria kuhusu uhifadhi wa mazingira ni kazi muhimu. Mbali na hayo tutaanzisha ukaguzi kuhusu sheria ya kinga ya uchafuzi wa mazingira, na kurekebisha sheria hiyo ili kutoa uhakikisho wa kisheria kwa kazi ya kushughulikia uchafuzi wa hewa."

    Mkutano huo na waandishi wa habari umeanza kwa Bibi Fu ying kuliwakilisha bunge la umma la China kulaani vikali tukio la kigaidi lililotokea tarehe 1 Machi, kuwakumbuka watu waliouawa katika tukio hilo, kutoa pole kwa watu walioathiriwa. Anasema :

    "ugaidi unafanyika bila ya kujali mipaka ya nchi. Tunatumai kuwa China itapata uelewa na ushirikiano kwa wingi zaidi kutoka kwa jumuiya ya kimataifa wakati inapofanya juhudi za kupambana na ugaidi."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako