• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping ataka wananchi wa makabila mbalimbali wathamini hali ya mshikamano

    (GMT+08:00) 2014-03-04 19:45:22

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa, wananchi wa makabila mbalimbali nchini China wanatakiwa kuthamini mshikamano kati ya makabila, na kupinga kithabiti maneno na vitendo vinavyoharibu mshikamano huo. Rais Xi amesema hayo aliposhiriki katika majadiliano kwenye Mkutano wa pili wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China.

    Katika hotuba yake, rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, kazi ya makabila inahusisha hali ya jumla ya nchi, na serikali inatakiwa kuharakisha mchakato wa kuendeleza uchumi na jamii katika sehemu wanapoishi watu wa makabila madogo madogo, ili kuwawezesha wananchi wa sehemu hizo kupata manufaa halisi.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesisitiza kuwa, ni lazima kudhibiti hali ya jumla ya nchi, kukusanya mapendekezo kwa pande zote, kuweka mipango inayohusika, na kudumisha mwelekeo mzuri wa hali ya uchumi inayopata maendeleo kwa utulivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako