• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yalenga ongezeko la uchumi la asilimia 7.5 kwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2014-03-05 10:51:26

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametangaza kuwa China imeweka lengo la ongezeko la uchumi kuwa asiliami 7.5 kwa mwaka huu, sawasawa na kiwango cha mwaka jana.

    Alipotoa ripoti ya yake ya kwanza ya kazi ya serikali kwa wabunge karibu 3000 kutoka kote nchini kwenye mkutano wa bunge la umma la China wa mwaka huu uliofunguliwa leo jijini Beijing, Bw. Li amesema lengo hilo limetolewa baada ya kuangalia mahitaji na uwezekano wote na kufanya ulinganishaji kwa makini.

    Ripoti hiyo ya kazi ya serkali inatolewa miezi minne baada ya China kuweka mpango wa mageuzi mfululizo katika nyanja mbalimbali mwishoni mwa mwaka jana.

    Huu ni mwaka wa tatu mfululizo kwa serikali ya China kuweka lengo la ongezeko la uchumi kuwa asilimia 7.5, kwani nchi hiyo inadhamiria kupeleka uchumi wake kwenye njia ya maendeleo endelevu.

    Aidha, ripoti hiyo inasema lengo la ongezeko la biashara ya China na nje kwa mwaka huu ni asilimia 7.5, huku kazi za kuboresha mwundo wa mauzo ya bidhaa nje ya nchi na kuhimiza uwiano katika ongezeko la biashara na nje zitapewa kipaumbele na serikali ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako