• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya China yaweka mipango mipya kuhusu kazi ya mwaka 2014

    (GMT+08:00) 2014-03-05 18:14:12

    Mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China ambacho ni chombo cha juu cha utungaji wa sheria cha China umefunguliwa leo asubuhi mjini Beijing, ambapo viongozi wa chama na serikali ya China, pamoja na wajumbe karibu na elfu tatu wa bunge hilo wanashiriki. Mkutano huo umeanza kwa wajumbe wote kuwakumbuka watu waliouawa katika tukio la kigaidi lililotokea usiku wa tarehe 1 Machi katika kituo cha treni kilichoko huko Kunming, mkoani Yunnan. Katika ufunguzi wa mkutano huo, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang akiwakilishi ya serikali ya awamu mpya ametoa ripoti ya kwanza ya serikali. Ripoti hiyo imesisitiza kuwa, mageuzi ya kazi kuu ya serikali ya China kwa mwaka huu. Anasema:

    "Inatakiwa kutoa kipaumbele kwa mageuzi ya mfumo wa uchumi huku tukihimiza mageuzi katika sekta zote kwa nia thabiti."

    Katika ripoti hiyo, Bw. Li Keqiang amekumbusha kazi ya serikali ya China katika mwaka uliopita kuhusu kuharakisha hatua ya kubadilisha majukumu ya serikali, kurekebisha muundo wa uchumi, kusukuma mbele hatua ya ufunguaji wa mlango, na kuhakikisha maisha ya wananchi kwa hatua halisi, mambo yote yameonesha mipango halisi ya mageuzi ya serikali ya awamu mpya.

    Kuhusu malengo ya maendeleo ya uchumi na jamii ya China ya mwaka 2014, ripoti hiyo imeeleza kuwa, thamani ya jumla ya uzalishaji nchini China inatakiwa kufikia asilimia 7.5, ongezeko la bei ya bidhaa kwa wananchi litadhibitiwa katika asilimia 3.5, ongezeko la idadi ya watu wanaopata ajira mijini na vijijini litazidi milioni kumi, na kiwango cha idadi ya watu wasio na ajira litadhibitiwa chini ya asilimia 4.6, uwiano kati ya mapato ya China kutokana na biashara ya nje na matumizi ya China katika nchi za nje utapatikana, aidha mapato ya wananchi na ongezeko la uchumi vitakuwa na maendeleo kwa pamoja.

    Bw. Li Keqiang amesisitiza kuwa, kudumisha ongezeko mwafaka la uchumi kuna umuhimu mkubwa kwa China. Akizungumzia namna ya kutimiza lengo hilo Bw. Li Keqiang anasema:

    "Mageuzi ya kazi kuu ya serikali kwa mwaka huu. Inatakiwa kuonesha haki na usawa na kuwawezesha wananchi wote kunufaika na mafanikio ya maendeleo ya mageuzi."

    Ripoti hiyo imeonesha kuwa, mwaka 2014 maendeleo mapya ya mageuzi yatahusisha sekta muhimu za mfumo wa utawala, ushuru na fedha. Wakati huo huo inasisitiza kuhimiza hatua ya ufunguaji mlango wazi. Bw. Li Keqiang anasema:

    "Inatakiwa kuanzisha mfumo mpya wa uchumi ulio wazi, kuhimiza hatua mpya za kufungua mlango wazi, ili kusukuma mbele hatua za mageuzi na kurekebisha muundo wa uchumi, na kuonesha sifa mpya katika ushindani wa kimataifa."

    Mbali na hayo, ripoti hiyo pia inafuatilia kazi ya kuboresha maisha ya wananchi, zikiwa ni pamoja na utoaji wa nafasi za ajira, matibabu, usalama wa chakula. Pia inahusisha suala la uchafuzi wa mazingira kama anavyoeleza Bw. Li Keqiang:

    "Eneo linaloathiriwa na uchafuzi wa hewa linazidi kupanuka, hili ni tishio linalotolewa na mazingira kwa njia isiyo mwafaka ya kujiendeleza kiuchumi. Ni lazima kuimarisha kuhifadhi mazingira ya asili, na kutekeleza kwa makini mipango ya utekelezaji wa kinga ya uchafuzi wa hewa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako