• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyombo vya habari duniani vyafuatilia mkutano wa baraza la bunge la umma la China

    (GMT+08:00) 2014-03-05 19:26:15

    Mkutano wa pili wa bunge la 12 la umma la China umefunguliwa leo hapa Beijing, na unafuatiliwa na vyombo mbalimbali vya habari duniani.

    Gazeti la Financial Times la Uingereza limesema, mambo yanafuatiliwa zaidi kwenye mkutano huo ni jinsi serikali ya China itakavyoshughulikia uwiano kati ya ongezeko la uchumi na ubebaji wa madeni, uwiano kati ya mageuzi na utulivu, uwiano kati ya uchumi na mazingira, na uwiano kati ya maumivu ya muda mfupi na manufaa ya muda mrefu. Shirika la habari la Reuters linasema, kazi muhimu zaidi ya serikali ya China ni kuhakikisha uchumi unaendelea kwa usalama na utulivu.

    Gazeti la Wall Street linasema, China imethibitisha lengo lake la ongezeko la uchumi kuwa ni asilimia 7.5 kwa mwaka huu. Katika miongo iliyopita, dunia inategemea ongezeko la uchumi wa China lililofikia karibu asilimia 10 kila mwaka, sasa China inataka kuonesha kuwa hali imebadilika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako