Kampuni ya Anglo American Platinum Amplats imetangaza kuwa, mazungumzo yanayolenga kusimamisha mgomo wa wachimbaji madini wa Platinum nchini Afrika Kusini yamesimamishwa. Taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo inasema kusimamishwa kwa mazungumzo hayo kutatoa muda kwa wahusika kutafakari madai ya sasa. Mazungumzo kati ya makampuni ya uchimbaji madini ya Platinum na shirikisho la wachimbaji na umoja wa ujenzi (AMCU) yalianza tarehe 24 Januari. AMCU ilitaka mshahara wa kila mwezi ufike dola 1136 za kimarekani, matakwa hayo yalikataliwa na makampuni ya wachimbaji madini. Jumanne AMCU ilirekebisha matakwa yao na kukubali lengo lake linaweza kutimizwa hatua kwa hatua ndani ya miaka minne. Kampuni ya Amplats inasema inafahamu marekebisho ya matakwa hayo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |