• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya asilimia 90 ya kampuni za nchi za nje zapenda kupanua uwekezaji nchini China

    (GMT+08:00) 2014-03-07 17:22:35

    Uchunguzi umeonesha kuwa, zaidi ya asilimia 90 ya kampuni zanchi za nje nchini China zinapenda kuongeza uwekezaji nchini China, kwani vivutio vya China kwa mitaji ya kigeni havibadiliki.

    Waziri wa biashara wa China Bw. Gao Hucheng amesema hayo wakati akizungumzia wasiwasi wa nchi za nje kuhusu mazingira ya uwekezaji nchini China kubadilika na kuwa mabaya.

    Takwimu kutoka Wizara ya biashara ya China zimeonesha kuwa, mwaka 2013 thamani ya matumizi ya fedha za kigeni ya China ilizidi dola za kimarekani bilioni 117.5, hili ni ongezeko la asilimia 5.25 kuliko mwaka 2012. Bw. Gao Hucheng ameeleza kuwa, mwaka jana kiwango cha jumla cha ongezeko la uwekezaji duniani kilikuwa chini ya asilimia 5.25, lakini China inadumisha ongezeko la kasi.

    Ili kuzidi kuboresha mazingira ya uwekezaji, Bw. Gao Hucheng amesema, China itafanya utafiti kuhusu hatua za ufunguaji mlango kwa nje katika kipindi kijacho, na hatua hizo zitahusisha sekta za fedha, elimu, utamaduni, matibabu, utoaji wa huduma kwa watoto na wazee, pamoja na mambo ya utengenezaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako