• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahimiza kuanzisha benki ya uwekezaji wa ujenzi wa miundo mbinu ya Asia 

    (GMT+08:00) 2014-03-07 18:35:09

    Waziri wa fedha wa China Bw. Lou Jiwei leo amesema, mchakato wa kuanzisha benki ya uwekezaji wa ujenzi wa miundo mbinu ya Asia uliopendekezwa na China unaendelea, na benki hiyo itatia nguvu mpya zaidi kwa ajili ya umoja na maendeleo ya uchumi wa nchi za Asia.

    Bw. Lou amesema Oktoba mwaka jana, kiongozi wa China alitoa wito wa kuanzisha benki hiyo, na kuitikiwa na nchi nyingi za Asia. Tarehe 24 Januari mwaka huu, China na nchi nyingine zaidi ya 10 za Asia zilifanya mkutano wa kwanza kuhusu kuanzishwa kwa benki hiyo, na hivi sasa China imeunda kikundi cha watu wanaoshughulikia maandalizi ya benki hiyo ili kuharakisha mchakato wa uanzishwaji wake.

    Benki ya uwekezaji wa ujenzi wa miundo mbinu ya Asia itakuwa shirika la kuhimiza maendeleo kati ya serikali za nchi za kikanda, na itaanza kwa mtaji wa dola za kimarekani bilioni 50 kutoka kwa nchi wanachama wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako