• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapinga wabunge wa bunge la Marekani kukutana na Dalai Lama

    (GMT+08:00) 2014-03-07 21:13:56
    China imepinga vikali na kulaani vikali kitendo cha baadhi ya wabunge wa bunge la Marekani kukutana na Dalai Lama.

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Qin Gang amesema, China inaitaka Marekani kuheshimu ahadi yake ya kuitambua Tibet kama sehemu ya China, na haiungi mkono kile kinachoitwa uhuru wa Tibet. Amesema kutokana na maneno na vitendo vya Dalai Lama katika miongo iliyopita, ni wazi kuwa ni mkimbizi wa kisasa ambaye amekuwa akijihusisha na vitendo vya kujitoa chini ya mwamvuli wa kidini.

    Amelitaka baraza la juu la bunge la Marekani kuacha kuingilia kati mambo ya ndani ya China kupitia suala la Tibet, na kuacha kuchochea au kuunga mkono vitendo vya kujitenga vinavyofanywa na baadhi ya nguvu za uhuru wa Tibet.

    Mwezi uliopita, Dalai Lama alikutana na rais Barack Obama wa Marekani, na alhamisi wiki hii, Dalai alirejea tena nchini humo kutoa sala inayoongoza vikao vyote vya bunge la juu la Marekani, kabla ya kukutana na viongozi wa ngazi ya juu wa bunge hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako