• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasisitiza kuendelea kufanya kazi ikiwa nchi kubwa inayowajibika

    (GMT+08:00) 2014-03-08 12:04:16

    Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amesema China itajitahidi kutoa mchango wake ikiwa nchi kubwa inayowajibika, kutetea haki na usawa katika mawasiliano ya kimataifa, hususan kulinda na kuendeleza maslahi za haki za nchi zinazoendelea, na kuchangia kazi ya kuboresha utararibu wa kimataifa ili uwe wa haki Zaidi.

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo hapa Beijing, Bw. Wang amesema mwaka huu, China itaimarisha uhusiano wa kirafiki na nchi mbalimbali duniani haswa nchi majirani, ili kuandaa mazingira mazuri kwa ajili ya kazi za kujiendeleza na mageuzi nchini China, na pia itaendeleza ushirikiano wa kunufaishana na nchi mbalimbali ili kuweka hali nzuri kwa kazi ya kubadilisha muundo wa uchumi wa China.

    Waziri huyo aliongeza kuwa, mkutano kuhusu uratibu na hatua za kujenga uaminifu barani Asia CICA na mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi ya Asia na Pasifiki APEC utakuwa ni kazi muhimu ya diplomasia ya China mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako