• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China kuizuru Afrika

    (GMT+08:00) 2014-03-08 12:57:08

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang atafanya ziara barani Afrika mwaka huu, na hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Bw. Li kufanya ziara barani Afrika tangu aingie madarakani mwaka jana.

    Hayo yamesemwa na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi akijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu uhusiano wa China na Afrika kwenye mkutano wa pili wa Baraza la 12 ya Bunge la Umma la China.

    Bw. Wang Yi alisema kwanza China na Afrika ni ndugu wazuri, wakati China ilipokuwa haijaondokana na umaskini, ilitoa msaada kwa Afrika katika harakati za kupigania uhuru na ukombozi, huku Afrika ikiisaidia Jamhuri ya Watu wa China katika juhudi za kurudishiwa nafasi yake halali katika Umoja wa Mataifa. Pili, China na Afrika ni marafiki wanaofanya ushirikiano kwa usawa. Amesema China siku zote inatilia maananani maslahi ya Afrika wakati inapofanya ushirikiano na Afrika, haiingilii kati mambo ya ndani ya nchi za Afrika na China imetimiza ahadi zote ilizotoa, na takwimu zinaonesha kuwa kwa jumla China imeisadia Afrika kujenga miradi zaidi ya elfu 1 bila ya kuweka masharti yoyote ya kisiasa. Tatu, China na Afrika ni wenzi wanaotafuta maendeleo ya pamoja. Amesema alipofanya ziara barani Afrika mwezi Januari mwaka huu, Waafrika wengi walimwambia kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika umechangia sana ukuaji wa uchumi wa Afrika kwa mufululizo katika miaka ya karibuni, na pia umezihimiza nchi nyingine duniani ziongeze uwekezaji barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako