• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jaji mkuu wa China aahidi kupambana na ugaidi

    (GMT+08:00) 2014-03-10 18:52:45

    Jaji mkuu wa China, Zhou Qiang, ameahidi kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa wa ugaidi, akitolea mfano tukio la shambulizi lililotokea kwenye kituo cha treni mjini Kunming.

    Zhou amesema hayo alipokuwa akiwasilisha ripoti ya kazi za mahakama kuu ya watu wa China katika kikao cha pili cha mkutano wa 12 wa bunge la umma la China. Amesema mahakama nchini China zitafanya kazi kikamilifu kulinda usalama wa taifa na utulivu wa jamii, pia kuongeza imani ya watu kuhusu usalama. Amesema mahakama zitatoa adhabu kali kwa wahalifu wanaovuruga usalama wa taifa, hususan wale wanaofanya mashambulizi ya kigaidi, wanaoleta tishio kwa usalama wa jamii na kuharibu vifaa vya kijesh

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako