Mapigano yanayoendelea kati ya jeshi la serikali ya Syria na makundi ya wapiganaji katika mkoa wa kaskazini maghaibi wa Latakia nchini Syria yamesababisha vifo vya zaidi ya waasi 500 tangu ijumaa iliyopita.
Gazeti la al-Watan la Syria limesema, wengi wa wapiganaji hao waliouawa ni raia wa Saudi Arabia na Chechniya, na kwamba waasi hao wameshindwa kudhibiti eneo lolote walilolenga, ikiwa ni kinyume na taarifa ambazo makundi hayo yanazitoa kwa vyombo vya habari.
Gazeti hilo limesema, waasi wanafanya mashambulizi ya ghafla mjini Kasab lakini hawajafanikiwa kudhibiti eneo lolote mjini humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |