• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuchunguza mauaji ya mhubiri mwenye ikitikadi kali Sheikh Makaburi

    (GMT+08:00) 2014-04-03 11:08:21

    Serikali ya Kenya imeanzisha uchunguzi wa mauaji ya mhubiri mwenye itikadi kali Abubakar Sheriff ambaye pia anafahamika kama Makaburi aliyeuawa kwa kupigwa risasi jumanne usiku mjini Mombasa. Mkuu wa polisi wa Kenya David Kimaiyo amemtaka mtu yeyote aliye na habari kuhusu tukio hilo kuwaarifu polisi ili wahusika wakamatwe. Kimaiyo amewataka makamanda wa polisi kuongeza juhudi za kuimarisha usalama kote nchini humo. Kauli hiyo inakuja wakati serikali za Uingereza na Marekani zimetoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa kina kuhusu matukio ya ukosefu wa usalama mjini Mombasa ili kuwakamata wahusika wa vitendo hivyo vya uhalifu. Wakati huo huo, hali ya tahadhari imeendelea kushuhudiwa mjini Mombasa kufuatia mauaji ya Makaburi, huku polisi wakionekana kuimarisha usalama katika makazi ya watu. Makaburi alikuwa mshirika mkubwa wa mhubiri mwenye itikadi kali Sheikh Aboud Rogo ambaye pia alipigwa risasi na kuuawa na watu wasiojulikana mwaka wa 2012.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako