Baraza la juu la bunge la Marekani limepiga kura kumzuia balozi mpya wa Iran kwenye Umoja wa Mataifa kuingia nchini humo kutokana na kuhusika kwake na kuwateka raia 52 wa Marekani mwaka 1979.
Baraza hilo limeipigia kura hoja iliyowasilishwa na mbunge wa Texas Ted Cruz inayodai kuwa, Hamid Aboutalebi, ambaye ni balozi mpya wa Iran kwenye Umoja wa Mataifa, ni mwanachama wa kundi la watu wenye silaha lililovamia ubalozi wa Marekani mjini Tehran Novemba 4 mwaka 1979 na kuwateka nyara raia 52 wa Marekani kwa muda wa siku 444.
Habari zinasema, Aboutalebi ameomba visa ya Marekani, na msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya nchi hiyo Marie Harf amesema, uteuzi huo ni wa utatanishi. Ameongeza kuwa Marekani imewasilisha wasiwasi wake kuhusu suala hilo kwa serikali ya Iran.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |