• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yafuatilia matukio ya kudai kujitawala katika maeneo ya mashariki mwa Ukraine

    (GMT+08:00) 2014-04-08 17:43:32

    Watu wanaoiunga mkono serikali ya Russia katika maeneo ya mashariki na kusini mashariki mwa Ukraine wamefanya maandamano na hata kushambulia na kukalia baadhi ya majengo ya serikali. Watu hao kutoka Donetsk na Kharkiv wamedai kuanzisha "jamhuri inayojitawala" na kufanyika upigaji kura za maoni. Jumuiya ya kimataifa inafuatilia machafuko mapya yanayotokea katika maeneo hayo nchini Ukraine,

    Mbunge wa mji wa Donetsk jana alisema bunge la mji huo limefanya mkutano na kupitisha kwa kauli moja azimio la kuanzisha "Jamhuri inayojitawala ya Donetsk". Wakati huohuo, kamati ya raia ya Donetsk imetangaza kuwa itafanya upigaji kura za maoni kuhusu kujiunga na Russia kabla ya tarehe 11 Mei, na pia imemwomba rais Vladimir Putin wa Russia kutuma vikosi vya muda vya usalama kwenye mji huo ili kulinda usalama wa wakazi wa huko. Siku hiyo, wapinzani mjini Kharkiv ambao ni mji wa pili kwa ukubwa nchini Ukraine pia walitangaza kuanzisha "Jamhuri ya Watu wa Kharkiv", ambapo kamati ya Kharkiv imesema itakuwa ni chombo pekee halali na hatma ya Kharkiv itaamuliwa kupitia upigaji kura za maoni tu.

    Spika wa bunge la Ukraine anayekaimu madaraka ya rais Bw. Oleksander Turchynov amesema hali ya wasiwasi katika maeneo hayo imeharibu utulivu wa taifa na inalenga kupindua utawala wa serikali ya Ukraine, na vitendo vya kukalia vyombo vya kiserikali vya Donetsk, Kharkiv na Luhanska vinachochewa na serikali ya Russia. Ametangaza kuwa Ukraine itaanzisha kikosi cha kutatua mzozo na kuchukua hatua za kupambana na ugaidi dhidi ya watu wanatumia nguvu na kufanya uchochezi katika maeneo hayo.

    Hata hivyo Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imeilaanni Ukraine kwa kauli hiyo na kusema haitafanya mageuzi ya katiba na kutekeleza mfumo wa jamhuri kulinda maslahi na uhuru wa sehemu mbalimbali, na kama haitarekebisha hadhi maalumu ya Kirusi katika maeneo hayo, Ukraine itashindwa kulinda utulivu wake. Russia imesema kama Ukraine inaendelea kupuuza hatma ya taifa na wananchi wake, itakabiliwa na changamoto nyingi zaidi, na inapaswa kuacha kauli yake kwamba matatizo ya Ukraine yanasababishwa na Russia.

    Kwa mujibu wa pendekezo la Ukraine, waziri wa mambo ya nje wa Russia Bw. Sergei Lavrov alizungumza na mwenzake wa Ukraine Andrey Deshchica kwa njia ya simu, ambapo Russia iliihimiza serikali ya Ukraine kuchukua hatua za dharura kukabiliana na hali ya wasiwasi katika eneo la kusini mashariki mwa Ukraine, kuhimiza mageuzi ya katiba na kuheshimu matakwa ya wananchi wa huko.

    Akizungumzia hali ya wasiwasi katika maeneo hayo ya Ukraine, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Jen Psaki amesema Russia, Ukraine, Marekani na Umoja wa Ulaya zitafanya mazungumzo ya moja kwa moja kuhusu hali ya Ukraine ndani ya siku kumi zijazo. Aidha, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw John Kerry alizungumza na mwenzake wa Russia Bw Lavrov kwa njia ya simu, ambapo Bw Kerry alisema Marekani inaitaka Russia ipinge hadharani vitendo vya watu wanaoleta mfarakano na uharibifu, na kuchukua hatua kutuliza hali ya wasiwasi. Msemaji wa ikulu ya Marekani Jay Carney amesema machafuko yanayotokea katika miji mingi mashariki mwa Ukraine yanatokana na shinikizo lililowekwa na Russia kwa Ukraine, na Marekani imeonya tena vikali dhidi ya vitendo vya Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako