• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Washington-Wizara ya fedha ya Marekani yakataa kuitaja China kama nchi inayoshusha thamani ya fedha yake kwa makusudi

    (GMT+08:00) 2014-04-16 18:26:37

    Wizara ya fedha ya Marekani jana imesema China haiwezi kuhesabiwa kama nchi inayoshusha kwa makusudi thamani ya fedha yake, lakini kasi ya thamani yake bado hairidhishi.

    Ripoti ya nusu ya kwanza ya mwaka kuhusu sera za kimataifa za uchumi na viwango vya mabadilishano ya fedha iliyotolewa na wizara ya fedha ya Marekani kwenye bunge la nchi hiyo imesema, thamani ya sarafu ya China RMB kwenye mambo ya biashara kwa mwaka jana ilikuwa inaridhisha, lakini haikuongezeka kwa kasi kama inavyohitajika.

    Hata hivyo, ripoti hiyo imesema, kupanuka kwa sekta ya biashara kunatoa fursa kwa China kupunguza uingiliaji na kuliruhusu soko kuchukua nafasi kubwa zaidi katika kuamua kiwango cha mabadilishano ya fedha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako