• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatakiwa kuwekeza kwa mradi wa kawi ya upepo

    (GMT+08:00) 2014-04-16 19:22:15

    Tanzania- Serikali ya Uingereza imeiomba ile ya Tanzania kuharakisha mchakato wa kuanzishwa kwa mradi wa kawi ya upepo katika eneo la Singida ili kupunguza tatizo la stima nchini humo.

    Wito huo ulitolewa na waziri wa kawi wa uingereza bwana Gregory Barker, alipotembelea eneo ambalo limetengwa kwa ajiili ya kuzalisha kawi hiyo viungani mwa mji wa Singida.

    Akiongea kwenye ziara hiyo naibu waziri wa kawi nchini Tanzania Stephen Maselle, aliwataka maafisa wa shirika la umeme nchini humo (TANESCO) kukamilisha mazungumzo kati yao na mwekezaji ili kuanza utekelezaji wa mradi huo.

    Kulingana na Maselle Tanzania inatarajia kuzalisha kati ya megawati 2,700 na 3,000 ifikapo mwkaa wa 2015.

    Kwa sasa Tanzania inazalisha megawati 1,500 pekee na mara kwa mara inakubwa na matatatizo ya kupotea kwa stima haswa kwenye viwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako