• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sekta ya sukari Tanzania yaathiriwa na magendo.

    (GMT+08:00) 2014-04-16 19:23:20

    Tanzania - Sekta ya sukari nchini Tanzania imeathiriwa na kuongezeka kwa uagiziaji wa kupita kiasi wa bidhaa hiyo kutoka nje.

    Wadau wa sukari nchini humo wanasema sukari nyingi inaangiziwa kutoka nje kwa njia za magendo na bei yake ni ya chini jambo ambalo linaadhiri viwanda vya ndani ya nchi.

    Mwezi jana viwanda nchini humo vilikuwa na hadi tani 62,800 za sukari ambazo havingeweza kuuza kwani soko limefurika sukari hiyo ya magendo.

    Taakwimu kutoka kwa halmashauri ya sukari nchini humo zinaonyesha kwamba zaidi ya tani 100,000 zimeingizwa nchini Tanzania licha ya serikali kupiga maruuku uagiziaji wa sukari kuanzia mwezi Januari.

    Mapema mwezi huu mamlaka ya ushuru nchini humo ilinasa tani 15 za sukari iliokuwa imeagizwa kimagendo kutoka Brazil kupitia kwa Bandari ya Bagamoyo.

    Waziri wa uwekezaji Bi. Mary Nagu anawataka wale wanaoagizia sukari kuzingatia kufungua viwanda nchini Tanznaia ili kulinda viwanda vya ndani ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako