• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali yawekeza shilingi milioni 400 kufufua kiwanda cha nguo cha Rivatex

    (GMT+08:00) 2014-04-16 19:23:57

    Kenya-Serikali ya Kenya imewekeza zaidi ya shilingi milioni 400 kufufua kiwanda cha nguo cha Rivatex kilichoko mjini Eldoret.

    Hayo ni kwa mujibu wa waziri wa viwanda Adan Mohammed alipozuru kiwanda hicho.

    Waziri Mohhamed alisema fedha hizo zitatumika kununua mashine mpya za kiwanda hicho ambacho sasa kinasimamiwa na chuo kikuu cha Moi.

    Alisema ukarabati wa kiwanda hicho ni muhimu kwani kina uwezo wa kufungua nafasi nyingi za ajira.

    Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago alisema ufufuzi wa Rivatex ni hatua muhimu ya kukuza uchumi wa kitaifa na pia kuchochea ukuaji wa upanzi wa pamba ambao ni mali gafi ya kuzalisha nguo.

    Alitoa wito pia kwa serikali na taasisi nyingine za serikali kununua manguo kutoka kwa kiwanda hicho kama ilivyokuwa awali kabla ya kudorora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako