• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya vyuo na madarasa 1,000 ya Confucius yaanzishwa duniani

    (GMT+08:00) 2014-04-17 18:33:05

    Ripoti iliyotolewa leo hapa Beijing kuhusu hali ya maendeleo ya utamaduni wa China kwa mwaka 2013 imeonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, vyuo 440 na madarasa 646 ya Confucius yameanzishwa katika nchi na sehemu 120 duniani. Chuo cha Confucius kimekuwa chapa ya kiutamaduni ya kueneza lugha ya Kichina na kuonesha ushawishi wa China.

    Habari zinasema mwaka jana idadi ya wageni waliojifunza lugha ya Kichina ilifikia milioni 150, ambayo imeongezeka kwa asilimia 50 kuliko ile ya mwaka 2010.

    Ripoti hiyo pia inasema, mwaka jana thamani ya mauzo ya bidhaa za utamaduni nje ya China ilifikia zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 9, kiasi ambacho ni ongezeko la asilimia 10.8 kuliko mwaka 2012.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako