Ziara ya kikombe cha dunia inayodhaminiwa na Coca Cola imefikia ukingoni baada ya kumaliza kutembezwa duniani, siku 52 tu kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza kutimua vumbi huko nchini Brazil. Baada ya kutembezwa katika nchi 89 ndani ya siku 221, kikombe hicho kwa sasa kipo kwenye safari yake ya mwisho huko Brazil, ambapo kitatembezwa kwenye miji 27 ndani ya wiki sita zilizosalia ili watu wa huko nao wakione kikombe hicho. Safari ya kikombe hicho nchini Brazil inaanzia leo jumanne na kutarajiwa kumalizia katika mji unaoandaa michuano hiyo wa Sao Paulo ambayo itakuwa siku ya ufunguzi juni 12.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |