Kenya itaanza tena kutoa leseni za utafutaji wa mafuta kwenye vitalu vipya baada ya sheria mpya kuhusu mafuta kukamilika. Mwanajiolojia mwandamizi katika wizara ya nishati Bw. Hudson Andambi, amesema kati ya vitalu 46 vya mafuta nchini Kenya, 41 tu vinafanyiwa utafutaji.
Kwenye maonesho ya tatu ya mafuta ya Afrika mashariki Bw. Andambi amesema Benki ya Dunia inaisaidia Kenya kufanya ukaguzi kamili kuhusu sheria za sekta ya mafuta nchini humo. Serikali ya Kenya ilitoa agizo la kusimamisha utafutaji wa mafuta kwenye vitalu vipya kwa miezi kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
xia,fadhili,xie
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |