• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang atoa hotuba katika makao makuu ya Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2014-05-05 22:13:44

    "Hamjambo? nafurahi sana kuwa hapa Addis Ababa inayosifiwa kuwa ni mji mkuu wa kisiasa wa bara la Afrika, na kutoa hotuba kwenye jumba la mkutano la Umoja wa Afrika ambalo ni alama ya urafiki kati ya China na Afrika. Nawashukuru mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Bi. Nkosazana Dlamini-Zuma na waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Hailemariam Desalegn kwa hotuba zenu zenye upendo na uchangamfu, namshukuru mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa Afrika rais Abdelaziz kwa kunialika, na naishukuru serikali ya Ethiopia na kamati ya Umoja wa Afrika kwa mapokezi ya ukarimu. Kwa niaba ya serikali ya China na wananchi wake, napenda kutoa salamu za dhati na matumaini mema kwa ndugu zetu wa Afrika!

    Hii ni ziara yangu ya kwanza barani Afrika tangu niteuliwe kuwa waziri mkuu wa China, na pia ni mara yangu ya pili kutembelea katika bara hili. Wachina wa rika yangu tumekua tukisikiliza hadithi kuhusu harakati za waafrika kupigania uhuru na kufuatilia habari kuhusu ujenzi wa reli ya TAZARA. Miaka nitano iliyopita, nilienda Misri ambayo ni maskani ya farao, leo nimekuja Ethiopia ambayo ni "kilele cha Afrika", nimejisikia kwamba watu wa China na wa Afrika wamekuwa na uzoefu wa kihistoria unaofanana, majukumu ya kimaendeleo yanayofanana, na ndoto moja ya kiroho. Nchi za Afrika zimepata maendeleo mapya kwa kujitegemea, ambayo ni mafanikio ya kufurahisha, na ushirikiano kati ya China na Afrika umepiga hatua za kufikia ngazi mpya, na kuwa na mustakbali mzuri. Afrika ye leo ina nguvu na uhai, imekuwa sehemu muhimu ya jukwaa la kisiasa na kiuchumi la dunia, naona Afrika imekuwa ncha moja ya dunia katika pande tatu.

    Kwanza, Afrika ni ncha muhimu katika jukwaa la kisiasa la dunia. Bara la Afrika lina nchi 54, ambazo ni robo ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, na zinatoa mchango muhimu katika kulinda amani na utulivu duniani. Uwezo wa nchi za Afrika unaendelea kuongezeka, mchakato wa utandawazi barani Afrika umepiga hatua, na nchi hizo zinatoa sauti moja na kushikilia msimamo mmoja katika masuala muhimu duniani yakiwemo maendeleo ya dunia, mabadiliko ya hali ya hewa na mageuzi ya mfumo wa usimamizi wa kimataifa. Katika hali ambayo nchi zinazoendelea zimejitokeza kwa pamoja, dunia nzima inapaswa kusikiliza sauti ya Afrika na kuheshimu michango iliyotolewa na Afrika. Afrika imekuwa nguvu muhimu katika kuhimiza dunia yenye ncha nyingi na demokrasia katika mahusiano ya kimataifa.

    Ya pili, Afrika ni ncha mpya katika ongezeko la uchumi duniani. Afrika ni bara kubwa, lina maliasili nyingi, watu wake wanafanya kazi kwa bidii, nguvu kubwa ya kuhimiza maendeleo kutokana na watu bilioni moja imeamshwa na kuonekana. Kuanzia karne hii mpya, uchumi wa Afrika umepiga hatua kwa haraka, ongezeko lake limezidi asilimia 5 kila mwaka, na kuifanya Afrika kuwa moja ya sehemu ambazo uchumi wake unaongezeka kwa kasi zaidi duniani, na kuifanya ing'are katika msukosuko wa fedha kimataifa. Thamani ya jumla ya uchumi wa Afrika imefikia dola za kimarekani trilioni 2, na kuifanya Afrika itambuliwe kuwa soko muhimu linalojitokeza duniani.

    Tatu, Afrika ni ncha yenye rangi nyingi katika ustaarabu wa binadamu. Afrika yenye historia ndefu na utamaduni unaong'ara ni chanzo cha ustaaraabu wa dunia yetu, na inatoa athari kubwa kwa utamaduni wa binadamu wa aina nyingi na mawasiliano kati ya utamaduni huo. Kutoka ugunduzi wa fuvu la binadamu wa kale Bibi Lucy, hadi mapiramid ya kale, kutoka ngoma za jadi hadi muziki wenye uchangamfu, vyote ni utambulisho mzuri wa Afrika. Sanaa za kisasa za aina ya muziki, uchongaji au uchoraji, zote zinang'arisha mwangaza wa ustaarabu wa Afrika.

    "Buibui wakikusanya nguvu zao wanaweza kumshinda Simba." methali hii ya kiethiopia inadhihirisha ukweli kwamba umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Afrika ya leo inapiga hatua kuelekea lengo la umoja kamili. Umoja wa Afrika wa leo unatoa mchango mkubwa zaidi katika mambo ya Afrika na ya dunia. Siku zote tuna heshimu watu wanaoishi katika bara hili, na tuna imani kwa mustakbali mzuri wa Afrika!

    Mabibi na mabwana,

    Katika miaka 50 iliyopita, waziri mkuu wa zamani wa China marehemu Zhou Enlai alifanya ziara katika nchi 10 za Afrika, ambapo alitoa hatua tano za China za kushughulikia mahusiano kati yake na nchi za Afrika na nchi za kiarabu, na kutoa kanuni nane kuhusu misaada ya kiuchumi na kiteknolojia ya China kwa nje. Ziara hiyo iliweka msingi imara kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika. Katika miaka 50 iliyopita, watu wa China na Afrika wameungana mkono na kusaidiana, na kujenga urafiki usiovunjika. Mshairi mmoja aliwahi kusema "anayecheka nawe, unaweza kumsahau, lakini unayelia nae utamkumbuka daima." Katika miaka ya 60 hadi 70, ili kuunga mkono nchi za kusini mwa Afrika kupigania uhuru na kuondoa ubaguzi wa rangi, watu wa China walijibana na kujenga reli ya TAZARA, na wachina 65 walipoteza maisha katika ujenzi wa reli hiyo ya uhuru. Ni sawa na wakati China iliporejeshwa uanachama katika Umoja wa Mataifa, ndugu zetu wa Afrika walitoa machozi ya furaha, na kushangilia kwamba huu ni ushindi mkubwa wa nchi zinazoendelea. Hii ni historia yetu ambayo inaonesha kuwa tuna mustakbali wa pamoja na kupigania ndoto ya namna moja, na ni mali ya kiroho ambayo tutaithamini daima, na pia ni msingi thabiti wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika katika siku zijazo.

    Baada ya kuingia karne mpya, hali ya kuaminiana kati ya China na Afrika imeendelea kuimarika, mawasiliano ya ngazi ya juu kati ya pande hizo mbili yameongezeka, ushirikiano kati ya pande hizo mbili umepata maendeleo mzuri, uhusiano ambao umekuwa mfano wa kuigwa kwa ushirikiano wa kusini-kusini. Rais Xi Jinping wa China alifanya ziara barani Afrika kwa mafanikio, na kuinua uhusiano wa wenzi wa kimkakati kati ya China na Afrika kufikia ngazi mpya. Mwaka 2013, thamani ya biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 210.2, ambayo ni mara zaidi ya 2000 kuliko ile ya mwaka 1960, China imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara wa Afrika kwa miaka mitano mfululizo. Uwekezaji wa moja kwa moja kutoka kwa China barani Afrika umefikia dola za kimarekani bilioni 25. Uwezekaji huo unaendelea kuongezeka umeleta manufaa halisi kwa watu wa pande zote mbili. Historia na hali ya sasa vinaonesha wazi kuwa maendeleo ya China yanatoa fursa kwa Afrika, Afrika ikipiga hatua, China pia inanufaika. China na Afrika zikiendelea kwa pamoja, dunia itakuwa nzuri zaidi.

    Mabadiliko mengi yanatokea katika dunia kwa hivi leo. Umoja wa Afrika umeweka Ruwaza ya maendeleo ya mwaka 2063, ambayo ni mpango mkubwa wa maendeleo ya Afrika kwa miaka 50 ijayo. China imeanzisha mchakato mpya wa kuimarisha mageuzi kwa pande zote, ili kutimiza ndoto ya kustawisha taifa. China na Afrika zote zinakabiliana na majukumu ya kuleta mambo ya kisasa, na uhusiano kati ya China na Afrika umeingia kipindi kipya cha kihistoria. Mwaka jana rais Xi Jinping wa China alipofanya ziara barani Afrika, alieleza msimamo wa China kuhusu kuendeleza uhusiano na Afrika yaani "udhati, uhalisi, udugu na uwazi",China siku zote inashikilia mtizamo huo na inapenda kushirikiana na Afrika katika kusukuma mbele zaidi uhusiano kati ya China na Afrika.

    Naona, uhusiano kati ya China na Afrika ni uhusiano wa shida na raha, ni uhusiano wa kupigania maendeleo kwa pamoja na pia ni uhusiano wa kufundishana. Ili kuimarisha zaidi uhusiano huo, pande zote mbili zinapaswa kushikilia kanuni nne zifuatazo.

    Kwanza ni kutendeana kwa dhati. Ustaarabu wa China na Afrika unafanana, wote unatilia maanani hisia za kupenda maskani, wote unahimiza usawa na mshikamano, kwa hiyo sisi ni "majirani wa kiroho".

    Marehemu Nelson Mandela anayejulikana kama "mtoto wa Afrika" aliwahi kusema, "Ingawa nilipata mafunzo mengi ya kimagharibi, sijawahi kusahau mimi ni Mwafrika." Walimwengu wanamheshimu sana kutokana na moyo wake wa kutokubali kushindwa na kupigania usawa. China na Afrika, sote tuliwahi kuvamiwa na kukandamizwa vibaya na ukoloni na ubeberu, ndiyo maana tunajua kabisa umuhimu wa uhuru na usawa. Hatupendi kuwalazimisha wengine wakubali nia yetu wala hatuingilii mambo ya ndani ya wengine, tena tunatatua masuala yanayojitokeza katika ushirikiano kati yetu kwa njia ya kushauriana kwa usawa. China inashikilia msimamo wa kuipa Afrika msaada usioambatana na sharti lolote la kisiasa. Hayo yote yamekuwa ni msingi muhimu kwa China na Afrika kuendeleza urafiki kati yao.

    Pili ni kuongeza mshikamano na hali ya kuaminiana. Napenda kumnukuu mwanafalsaha mmoja Mchina wa zama za kale, akisema "Ukitaka kupendwa na wengine, wapenda kwanza. Ukitaka kupokelewa na wengine, wapokea kwanza." Kuheshimiana ni sharti la kwanza la kuwa na hali ya kuaminiana kisiasa. China na Afrika kila upande siku zote unaheshimu maslahi kuu na masuala yanayofuatiliwa na upande mwingine. China inashikilia kutetea haki mambo ya haki ya Afrika na matakwa yake halali, huku Afrika pia siku zote inaiunga mkono kithabiti China katika juhudi za kulinda haki na maslahi yake muhimu. Pande zetu mbili tunaweza kuimarisha uratibu na ushirikiano katika mambo ya kimataifa na kikanda, na tunatoa mchango katika juhudi za kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea. Katika jukwaa la kimataifa, China na Afrika zinaonekana kufuatilia masuala yanayofanana na kuwa na misimamo sawa, vile vile China na Afrika zinadumisha hali nzuri ya kushauriana. Miongoni mwa nchi zenye viti vya kudumu katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, China ni nchi inayoshiriki kwenye operesheni nyingi zaidi za ulinzi wa amani barani Afrika, ambapo walinzi amani wa China wanatekeleza majukumu katika sehemu kadha wa kadha za Afrika. kuwa na mshikamano na hali ya kuamaniana kwa China na Afrika, kunachangia juhudi za kujiendeleza za pande zetu mbili, pamoja na amani na maendeleo ya dunia nzima.

    Tatu ni kupata maendeleo kwa pamoja. China ni nchi inayoendelea yenye idadi kubwa zaidi ya watu na eneo kubwa zaidi duniani, huku Afrika ni bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea. China ina uwezo mkubwa katika sayansi na teknolojia, na mitaji, kwa upande wa Afrika, ina soko kubwa ambalo halijaendelezwa ipasavyo, na pia ina idadi kubwa ya nguvukazi. Tunaweza kusaidiana kiuchumi, na kila upande kunufaika na biashara zinazoendelea kwa hali motomoto siku hadi siku, hali ambayo inazifanya China na Afrika haziwezi kutengana. China inapenda kubadilishana uzoefu wa kujiendeleza na Afrika, kunufaika kwa pamoja na fursa ya kujiendeleza ili tupate maendeleo kwa pamoja. China inapenda kuipatia Afrika teknolojia za kisasa ilizobuni. Na China na Afrika kila upande unatakiwa kutumia vizuri nguvu yake bora ili ushirikiano wetu uwanufaishe watu wa pande zetu mbili. Kwa moyo wa dhati China inaunga mkono juhudi za Afrika za kupata wenzi wengi wa ushirikiano, inafurahia kuona jumuiya ya kimataifa iongeze uwekezaji na msaada kwa Afrika, China pia inapenda kushirikiana na upande wa tatu katika Afrika.

    Nne ni kutafuta njia mpya za ushirikiano halisi. Afrika ipo katika kipindi ambacho uchumi wake unaanza kukua kwa kasi na Afrika inajiunga na mchakato wa utandawazi wa uchumi duniani. China itaimarisha mageuzi na kuharakisha mchakato wa kubadilisha nji za kujiendeleza uchumi. Ushirikiano kati ya China na Afrika unaendana na mkondo mkuu wa dunia, na kila upande unatakiwa kuzingatia masuala yanayofuatiliwa na upande mwingine ili kutafuta na kupanua maslahi ya pamoja. Ushirikiano wetu haupaswi kuhusiana tu na sekta za nishati, maliasili na ujenzi wa miundo mbinu, bali pia unapaswa kupanuka hadi sekta nyingine nyingi kama vile viwanda, ukuaji wa miji na maendeleo ya kilimo cha kisasa. Ushirikiano huo unatakiwa kuzingatia kupigania maendeleo bila kuleta uchafuzi na kuhifadhi mazingira, unatakiwa kutumia vizuri nguvu zinazochanganywa za soko na sera za serikali, unatakiwa kuhamasisha viwanda vichangie zaidi shughuli za jamii, ili ushirikiano kati ya China na Afrika uwe mfano wa kuigwa kutokana na mafanikio yake na ufanisi wake.

    Mabibi na mabwana!

    Ushirikiano kati ya China na Afrika umepata mafanikio makubwa, na hivi sasa unafungua ukurasa mpya. Tuna maslahi mengi zaidi ya pamoja, msingi imara wa ushirikiano na fursa nzuri za kujipatia mafanikio zaidi. Tukitupa macho siku za baadaye, China inapenda kufanya juhudi pamoja na nchi za Afrika, kusukuma mbele utekelezaji wa miradi 6 mikuu, na kufanya ushirikiano wetu upige hatua mbele.

    Mradi wa kwanza ni ushirikiano katika sekta ya viwanda. Katika miaka ya karibuni, biashara kati ya China na Afrika inakua kwa kasi. Hivi sasa tunapaswa kuongeza ukubwa wa biashara hiyo na kuongeza ufanisi wake, ili biashara hiyo ifikie dola za kimarekani bilioni 400 hadi ifikapo mwaka 2020, na uwekezaji wa China barani Afrika uzidi dola bilioni 100. China itashiriki kwenye mchakato wa maendeleo ya viwanda barani Afrika, kuimarisha ushirikiano na Afrika katika viwanda vinavyohitaji nguvukazi nyingi kama vile nguo na vyombo vya umeme vinavyotumika nyumbani na shughli za utengenezaji, kusukuma mbele maendeleo ya sekta ya nishati na maliasili, kuisaidia Afrika iwe na uwezo zaidi wa kujiendeleza. Hali nzuri ya miundo mbinu ni msingi wa viwanda. China itashiriki kwenye ujenzi wa barabara, reli, mawasiliano ya habari na posta na umeme ili kuondoa vikwazo vya mawasiliano barani Afrika. Serikali ya China imetoa pendekezo la kutekeleza mradi wa ushirikiano wa usafiri wa ndege kati ya China na Afrika, ambapo China itaunga mkono mashirika yake yaingie ubia na wenzi wa Afrika kuanzisha mashirika ya ndege, China itatoa ndege za abiria na kuendeleza kwa pamoja sekta ya usafiri wa ndege ya Afrika.

    Mradi wa pili ni ushirikiano wa mambo ya fedha. China imeamua kuzidi kutoa mitaji yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 10 kwa nchi za Afrika, hali ambayo itafanya jumla ya mitaji iliyoahidiwa na China kufikia dola bilioni 30, fedha hizo zitatumika katika miradi ya kibiashara iliyokubaliwa na pande zetu mbili. Tunapenda kuona mitaji maalumu inayotolewa na viwanda vidogo vya Afrika na vyenye ukubwa wa kati itatumiwa ipasavyo, pia tunafanya mazungumzo na benki ya maendeleo ya Afrika katika kuanzisha mfuko wa pamoja utakaochangia ujenzi wa miundo mbinu barani Afrika. China inaunga mkono kuimarisha ushirikiano katika mambo ya fedha, kama vile ubadilishaji wa fedha, benki za kila upande kuanzisha matawi katika upande mwingine.

    Mradi wa tatu ni ushirikiano wa katika kuondoa umaskini. China ilipata mafanikio makubwa katika kuondoa umaskini katika miaka 20 iliyopita, hata hivyo kwa mujibu wa vigezo vya benki ya dunia, bado wapo watu maskini wapatao zaidi ya milioni 200 duniani. Afrika pia inakabiliwa na jukumu kubwa la kupambana na umaskini. Safari hii China na Umoja wa Afrika zitatangaza mwongozo wa kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika kuondoa umaskini, tunapenda kubadilishana uzoefu na nchi za Afrika katika kupunguza umaskini. China itaendelea kupeleka madaktari katika nchi za Afrika, na kuimarisha ushirikiano na Afrika katika mambo ya afya na matibabu. China ikishirikiana na Umoja wa Afrika na nchi mbalimbali za Afrika, itatekeleza mradi wa vielelezo vya kilimo, ili kuinua kiwango cha teknolojia za kilimo katika nchi za Afrika na kuongeza mavuno. Vile vile China itatekeleza mpango wa kutoa mafunzo ya kilimo kwa mafundi wapatao elfu 2 wa Afrika katika miaka mitano ijayo. Msaada wa China utatolewa haswa katika shughuli zinazohusiana na maisha ya Waafrika kama vile maji safi ya kunywa na kinga na matibabu ya magonjwa ya kuambukizwa.

    Nne, kutekeleza mradi wa ushirikiano wa kuhifadhi mazingira. Binadamu tuna dunia moja tu, kuhifadhi mazingira ni wajibu wetu wa pamoja. Afrika ina mazingira maalumu ya kimaumbile, ambayo yanatukumbusha watu zama za kale na mustakbali wa maisha mazuri. Ili kuhifadhi wanyamapori wa Afrika, serikali ya China itatoa msaada wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 10 kwa Afrika, kuimarisha ushirikiano wa teknolojia na kubadilishana uzoefu na nchi za Afrika. Vilevile tutaharakisha kujenga kituo cha utafiti wa pamoja cha China na Afrika nchini Kenya, katika masuala yanayofuatiliwa na nchi za Afrika yakiwemo kuhifadhi uwepo viumbe anuai, kuzuia na kushughulikia kuenea kwa jangwa na kutoa vielelezo vya kilimo cha kisasa, China na Afrika zitaimarisha ushirikiano katika sekta ya uhifadhi wa mazingira, kujitahidi kuendeleza nishati safi na nishati endelevu. Tunapaswa kujiendeleza huku tukihifadhi mazingira, na tuhifadhi mazingira huku tujiendeleze, ili China na Afrika ziendelee kwa pamoja.

    Tano, kutelekeza mradi wa ushirikiano wa mawasiliano ya utamaduni. Mawasiliano ya utamaduni ni mawasiliano ya moyoni, maelewano yatasaidia kuwepo kwa masikilizano. Tutaimarisha maingiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika, kutekeleza vizuri miradi mbalimbali ya mpango wa kiwenzi na ushirikiano wa kitamaduni kati ya China na Afrika, na shughuli za kirafiki zisizo za kiserikali kati ya China na Afrika. Kujenga zaidi vituo vya utamaduni vya China na vyuo vya Confucius barani Afrika, ili urafiki kati ya China na Afrika uwe mioyoni mwa watu.

    Watu wenye ujuzi wanasaidia kuleta ustawi wa dunia. China itahimiza kwa pande zote mpango wa kutoa mafunzo ya ujuzi kwa Afrika, kutimiza lengo la kuwapatia wanafunzi wapatao elfu 18 wa Afrika udhamini wa masomo wa serikali ya China na kutoa mafunzo kwa watu elfu 30 wa sekta mbalimbali.

    China imetoa msaada wa dola za kimarekani milioni 10 kwa kituo cha msaada wa kiufundi cha Afrika kinachoandaliwa na IMF, ili kuinua uwezo wa watu wa Afrika wa kutafuta ajira. .

    China inafanya ushirikiano wa elimu ya sayansi na teknolojia, kuimarisha mafunzo ya ufundi wa kazi, ili kuzisaidia nchi za Afrika kuboresha uwezo wa wafanyakazi. Tutawahamasisha wachina zaidi kuja kutalii barani Afrika, pia tunakaribisha watu wa Afrika kutalii, kusoma na kuwekeza nchini China.

    Sita, kutelekeza mradi wa ushirikiano katika kutafuta amani na usalama. Kama hakuna hali ya amani na tulivu, basi hakuna maendeleo. China inashikilia kuunga mkono nchi za Afrika kutatua masuala ya Afrika kwa njia ya kiafrika. Tutatekeleza kwa kina mapendekezo kuhusu kuendeleza uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano kati ya China na Afrika katika kutafuta amani na usalama, kujadili utoaji wa msaada kwa ujenzi wa jeshi la kudumu la Afrika na kikosi cha kuchukua hatua wakati wa kukabiliana na hali ya dharura, kuunga mkono ujenzi wa utaratibu wa pamoja wa usalama wa Afrika, na kushirikiana na Afrika katika kuwaandaa watu wenye ujuzi, kubadilishana habari za upelelezi , na kutoa mafunzo ya kijeshi, kusaidia Afrika kuongeza uwezo wa kulinda amani, kupambana na ugaidi na uharamia. Ili kusaidia Sudan Kusini kukabiliana na hali mbaya ya kibinadamu, China itatoa msaada wenye thamani ya Renminbi milioni 50.

    Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika ni uwanja muhimu kwa pande hizi mbili kuendeleza kwa kina uhusiano kati yao. Katika miaka iliyopita, baraza hili limekuwa likifanya kazi kubwa katika kuongeza mawasiliano na kuhimiza ushirikiano kati ya China na Afrika. Tunatakiwa kuendelea kukamilisha utaratibu huu, kuimarisha ushirikiano, ili kulifanya baraza hili liwe na ufanisi zaidi. Mwaka kesho itatimia miaka 15 tangu baraza hili lianzishwe, China inapenda kushirikiana na nchi za Afrika katika kuandaa mkutano wa 6 wa mawaziri, na kutoa hatua nyingi zaidi zinazolingana na mahitaji ya Afrika na China, ili ushirikiano kati ya China na Afrika uwe kwenye mstari wa kwanza wa ushirikiano na Afrika, na kuwa na mafanikio makubwa zaidi.

    Mabibi na mabwana!

    Ethiopia ni nchi yenye historia ndefu na ustaarabu mkubwa iliyo kwenye uwanda wa juu wa Afrika Mashariki. Nchi ya Ethiopia ambayo jua linachomoza kwa miezi 13 huko, na ni sehemu inayozalisha kahawa. Waethiopia ni watu wenye bidii na ushupavu , wanathamini uhuru na kuwa na desturi ya kupambana na uvamizi kutoka nje Ethiopia cha People's Revolutionary Democratic Front kimekuwa kinawaongoza Waethiopia kutafuta njia ya kujiendeleza inayoendana na hali halisi ya nchi yao. Sura ya nchi hii imekuwa imekuwa na mabadiliko makubwa . Ethiopia inatoa mchango mkubwa katika mambo ya Afrika. Tunawatakia Waethiopia mafanikio makubwa wakati mnaijenga nchi yenu.

    Phoenix, ambaye ni ndege mwenye maisha marefu katika hadithi za mapokeo za Afrika, anajiwasha moto kila baada ya miaka 500, na anazaliwa upya kutoka majivu. Pia kuna ndege kama huyu katika hadithi za mapokeo za China. Hadithi hizi zinazofanana zinatukumbusha kwa namna moja ulazima wa kihisitoria wa kufufuka kwa Afrika na kwa taifa la China. Mito hutiririka kuelekea baharini, upepo unavuma, ni wakati mzuri wa kung'oa tanga. Tutumie fursa tulizonazo, kushirikiana bega kwa bega katika kujenga mustakbali mzuri zaidi wa uhusiano kati ya China na Afrika. "

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako