• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China apendekeza kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika katika maeneo sita

    (GMT+08:00) 2014-05-06 10:19:41

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang amependekeza China na Afrika ziimarishe ushirikiano katika mambo ya viwanda, fedha, kupunguza umaskini, uhifadhi wa mazingira, mawasiliano kati ya watu na amani na usalama, ili kuufanya uhusiano kati ya pande mbili uingie kwenye kiwango kipya. Bw. Li Keqiang amesema hayo alipotoa hotuba kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa.

    Waziri mkuu wa Ethiopia Bw. Hailemariam Dessalegn na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bi. Nkosazana Dlamini-Zuma pia wametoa hotuba wakikaribisha na kusifu mpango wa ushirikiano kati ya Afrika na China uliotolewa na Bw. Li Keqiang, na kusema Afrika inapenda kuendelea kushirikiana na China, kuimarisha zaidi uhusiano kati yao na kutoa mchango kwa maendeleo ya pande hizo mbili na ya dunia nzima.

    Jana asubuhi, Bw. Li Keqiang, Bw. Hailemariam na Bi. Zuma walitembelea maonyesho ya reli na usafiri wa anga ya China yaliyofanyika katika kituo cha mkutano cha Umoja wa Afrika. Bw. Li Keqiang alisema China inapenda kushiriki zaidi kwenye ujenzi wa reli barani Afrika, na intarajia kujenga kituo cha usanifu wa treni ya mwendo kasi barani Afrika, kubadilishana uzoefu wa teknolojia na usimamizi, kupendekeza kuanzisha "mpango wa ushirikiano wa usafiri wa ndege kati ya China na Afrika", kuendeleza kwa pamoja sekta ya usafiri wa ndege ya Afrika ili kusaidia kuongeza mawasiliano barani Afrika

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako