• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China akutana na rais wa Ethiopia

    (GMT+08:00) 2014-05-06 20:10:51

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ambaye yuko ziarani nchini Ethiopia leo asubuhi kwa saa za huko amekutana na rais Mulatu Teshome wa Ethiopia.

    Bw. Li Keqiang amesema, China inapenda kuimarisha urafiki na ushirikiano kati yake na Ethiopia haswa katika sekta za ujenzi wa miundo mbinu, utengenezaji, viwanda na mambo ya fedha, na kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kufikia kiwango kipya.

    Rais Mulatu amesema, Ethiopia inapenda kuiga mfano wa China, kujifunza uzoefu wa kujiendeleza wa China, na kupanua ushirikiano kati yake na China katika sekta za ujenzi wa miundo mbinu. Amesema Ethiopia inayakaribisha makampuni ya China kuwekeza nchini humo, kuhimiza ongezeko na mageuzi ya uchumi wa Ethiopia, ili kutimiza maendeleo ya pamoja.

    Bw. Li Keqiang leo atamaliza ziara yake nchini Ethiopia na kuelekea Nigeria kuhudhuria mkutano wa 24 wa Baraza la uchumi duniani.

    (Upendo, Carol, Simba)

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako