• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China awasili Abuja kuanza ziara rasmi nchini Nigeria

    (GMT+08:00) 2014-05-07 10:03:15

    Waziri mkuu wa China Li Keqiang amewasili Abuja na kuanza ziara nchini Nigeria. Bw. Li Keqiang amesema uchumi wa Nigeria unashika nafasi ya kwanza kwa ukubwa barani Afrika, na Nigeria ni mwenzi muhimu wa China, mawasiliano kati ya viongozi wa nchi hizo mbili ni ya karibu na uhusinao wa wenzi wa kimkakati pia umeimarika. Amesema anapenda kufanya mazungumzo na kubadilishana maoni na viongozi wa Nigeria kuhusu masuala ya uhusiano wa pande mbili.

    Kutokana na mwaliko wa mwenyekiti wa Baraza la Uchumi Duniani Bw Klaus Schwab, Bw. Li Keqiang pia atahudhuria na kuhutubia Mkutano wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika utakaofanyika mjini Abuja, na kukutana na viongozi washiriki wa nchi za Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako