• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wasomi wa Afrika wasifu hotuba ya Waziri mkuu wa China aliyotoa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika

    (GMT+08:00) 2014-05-07 10:03:43

    Wasomi wa Afrika wamesifu hotuba ya Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang aliyotoa kwenye makao makuu ya Umoja wa Afrika, na kusema mipango aliyotoa kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya China na Afrika katika maeneo sita, kuboresha Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika na kuimarisha zaidi ushirikiano kati yao inakaribishwa na nchi za Afrika.

    Mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Sudan Mohammed Hassan Said amesema hotuba imeeleza kanuni, fikra na mipango halisi kuhusu jinsi ya kuimarisha na kusukuma mbele uhusiano kati ya China na Afrika, pamoja na maeneo yatakayofanyiwa ushirikiano.

    Msomi wa Zimbabwe Bw. Johnson amesema hotuba ya Bw. Li imeingiza mambo mapya na uhai kwenye ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuinuka kwa ushirikiano kati ya China na Afrika kunatarajiwa toka muda mrefu na nchi za Afrika. Amesema aliyotaja Bw. Li Keqiang kuhusu kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika yanalingana na mpango ya miaka 50 wa Afrika aliotoa mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Bibi Nkosazana Dlamini –Zuma.

    Aliyekuwa balozi wa Misri nchini China Bw. H.E. Ahmed Rezk amesema hotuba ya Bw. Li Keqiang imetoa taarifa nyingi muhimu, na cha muhimu ni kuwa viongozi wa China wataendelea kuunga mkono maendeleo ya nchi za Afrika.

    Msomi wa masuala ya maendeleo wa Zambia Bw. Fred Sumter amesema njia ya ushirikiano aliyopendekeza Bw. Li Keqiang ni fursa kwa nchi za Afrika, na kuhakikisha kuwa ushirikiano kati ya Afrika na China ni wa kusaidiana na kunufaisha pande mbili, na Afrika haitakuwa ni mtoaji wa raslimali tu, na China itasaidia Afrika kuongeza thamani ya ya bidhaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako