• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China asisitiza kuimarisha mawasiliano ya uchumi, biashara na utamaduni kati ya China na Afrika

    (GMT+08:00) 2014-05-07 09:43:02

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana alihudhuria mkutano kuhusu mawasiliano ya uchumi, biashara na utamaduni kati ya China na Afrika mjini Addis Ababa, ambapo wafanyabiashara kutoka kampuni mbalimbali za Ethiopia, Tanzania na Ghana walisema ushirikiano kati yao na kampuni za China umehimiza maendeleo ya kampuni zao, na wanatarajia kupanua sekta za ushirikiano, na kujipatia manufaa zaidi. Bw. Li Keqiang amesema, mawasiliano ya uchumi na biashara, na mawasiliano ya utamaduni yameungana na kuwa magurudumu yanayotarajiwa kusukuma mbele kwa kasi ushirikiano kati ya China na Afrika.

    Bw. Li Keqiang, akiongozana na rais Mulatu Teshome wa Ethiopia  walitembelea hospitali ya Alert mjini Addis Ababa, ambapo walitoa salamu kwa wagonjwa wa mtoto wa jicho waliofanyiwa upasuaji kwa bure kwa msaada wa China. Imefahamika kuwa kuanzia mwaka 2010, China imewafanyia upasuaji wagonjwa wa ugonjwa huo zaidi ya elfu 2 barani Afrika.

    Alasiri ya jumatatu Bw Li alihudhuria hafla ya kukamilisha kipindi cha kwanza cha ujenzi na kuzindua kwa kipindi cha pili cha ujenzi wa barabara ya kasi kutoka Addis Ababa hadi mji wa Adama. Imefahamika kuwa hiyo ni barabara ya kwanza katika Afrika Mashariki, inayojengwa na kampuni ya China kwa mujibu wa teknolojia na vigezo vya China.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako