• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka kampuni zake kuwekeza zaidi katika sekta ya viwanda nchini Nigeria

    (GMT+08:00) 2014-05-07 18:01:31

    China imevitaka viwanda vyake kupanua uwekezaji katika sekta ya utengenezaji nchini Nigeria, kuhamisha teknolojia, na kutoa mafunzo kwa wafanyakazi ili kuongeza nafasi za ajira nchini humo.

    Hayo yamesemwa leo na waziri wa biashara wa China Gao Hucheng. Amesema kutokana na Nigeria kuwa na idadi kubwa ya watu na soko kubwa la manunuzi, na China kuwa na uwezo mkubwa katika sekta ya uzalishaji, nchi hizo mbili zinaweza kuimarisha zaidi ushirikiano katika maeneo ya viwanda vya kutengeneza vitambaa, nguo, na vifaa vya umeme nyumbani.

    Nigeria ni nchi ya tatu kwa uwekezaji wa China barani Afrika, na hadi kufikia mwisho wa mwaka 2012, thamani ya uwekezaji huo imefikia dola za kimarekani bilioni 1.95.

    Gao amesema, katika miaka ya hivi karibuni, uwekezaji wa makampuni binafsi ya China nchini Nigeria umeongezeka, huku makampuni binafsi zaidi ya 40 ya China yakiwekeza dola milioni 800 za kimarekani nchini humo katika sekta za kilimo, viwanda vya nguo, vifaa vya ujenzi, madini na sekta nyingine.

    (Carol, Simba)

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako