• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa Afrika wa baraza la uchumi duniani wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2014-05-07 20:21:16

    Mkutano wa 24 wa kilele wa Afrika wa Baraza la uchumi duniani umefunguliwa leo huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria, ambapo washiriki zaidi ya 900 kutoka nchi zaidi ya 70 watajadili mustakabali na changamoto zinazoyakabili maendeleo ya uchumi wa Afrika.

    Kauli mbiu ya mkutano huo wa siku tatu ni kuhimiza ongezeko la pamoja na kuongeza nafasi za ajira.

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ambaye yuko ziara nchini Nigeria, atahudhuria mkutano huo na kutoa hotuba kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana kati ya China na Afrika, kuhimiza ongezeko la pamoja la uchumi wa Afrika, na kutimiza maendeleo ya pamoja ya China na Afrika.

    (Upendo, Carol, Simba)

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako