• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China Li Keqiang akutana na rais Jakaya Kikwete wa Tanzania

    (GMT+08:00) 2014-05-08 09:34:40

    Waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang amekutana na kufanya mazungumzo na rais Jakaya Kikwete wa Tanzania ambaye yupo mjini Abuja kuhudhuria Mkutano wa Uchumi Duniani kuhusu Afrika. Bw. Li Keqiang amesema katika miaka 50 iliyopita tangu China na Tanzania zianzishe uhusiano wa kibalozi, nchi mbili zinaheshimiana, kuaminiana na kuungana mkono katika masuala mbalimbali, na uhusiano kati yao unaongoza katika uhusiano kati ya China na nchi za Afrika. Amesema China na Tanzania zinaweza kusaidiana kupitia ushirikiano, na katika hali mpya, China inapenda kuimarisha mawasiliano ya ngazi ya juu na Tanzania, kupanua ushirikiano wa kunufaishana, kuandaa miradi mikubwa ya ushirikiano, kuongeza mawasiliano kati ya watu ili kuendeleza z ushirikiano.

    Rais Jakaya Kikwete amesema China ni rafiki anayetegemewa wa Tanzania na wa Afrika, na mapendekezo aliyotoa Bw. Li Keqiang kwenye hotuba yake kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Afrika yanalingana na mahitaji ya nchi za Afrika katika kujiendeleza na matarajio ya watu wa Afrika. Amesema Tanzania inapenda kuimarisha urafiki wa jadi na China, kuongeza ushirikiano ili kusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Bw. Li Keqiang pia amekutana na kufanya mazungumzo na rais Boni Yayi wa Benin, rais Faure Essozimna wa Togo na waziri mkuu wa Mali Bw. Moussa Mara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako