• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kusaidia kuwatafuta wasichana waliotekwa nyara nchini Nigeria

    (GMT+08:00) 2014-05-08 09:36:31
    China itatoa teknolojia ya kisasa ya utafutaji ili kusaidia idara za usalama za Nigeria kuwatafuta na kuwaokoa wanafunzi wasichana waliotekwa nyara nchini humo.

    Akizungumza na waandishi wa habari, mshauri maalum wa rais wa Nigeria Bw. Reuben Abati amesema waziri mkuu wa China ametoa ahadi hiyo kwenye mazungumzo na rais Goodluck Jonathan, akiahidi kutoa habari muhimu zinazohitajika kutoka kwenye satelaiti zake na mashirika yake ya kijasusi kwa idara za usalama za Nigeria.

    Bw. Abati ameongeza kuwa, Bw. Li Keqiang amesisitiza kuwa China itaiunga mkono Nigeria kwa njia zote katika juhudi za kupambana na ugaidi, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wanajeshi.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako